Tetesi: Bomba la mafuta Dar - Mwanza, muda si muda wenye matanki watauzia maji

Tetesi: Bomba la mafuta Dar - Mwanza, muda si muda wenye matanki watauzia maji

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
38,920
Reaction score
44,970
Nasikia kuna huu mradi wa bomba la mafuta from Dar to Mwanza, umefikia wapi? Na nini hatma ya wamiliki wa fuel tankers? Pia bei yake kwa Mwanza itashuka kwa lita?
Nadhani watalisogeza hadi Uganda ili kulifanya lilipe kwa haraka zaidi, ila napendekeza lile la mafuta lichimbiwe kwenye mtaro mmoja sawa na hili la gesi ili kupunguza gharama
TPDC yaanza mchakato ujenzi bomba la gesi Dar - Uganda - JamiiForums
 
Mimi kwa mawazo yangu sidhani kama inaweza kuwa tatizo. Najaribu kuwaza kwa upande wa Zambia lipo lile bomba la TAZAMA lakini tankers zaenda daily. Tena siku si nyingi kulikuwa na mgogoro kwamba Lorries za kutoka kwetu hapa ziache kwenda na mafuta kwenye tanks zao za akiba ili angalau wawe wanajaza kwenye petrol stations zao kule Zambia. Kama hamna tankers zinazopeleka mafuta huko niko tayari kusahihishwa katika hili.
 
TAZAMA pipeline lipo lakini kila siku Tanker's zinapasua anga kwenda Congo na Zambia..
 
hilo la TAZAMA mbona lipo miaka nenda rudi lakini mbona magari nayo yanasafirisha?
Naomba kuelimishwa kwa upole tu, ni kwamba bomba halitoshelezi mahitaji au tatizo ni uwezo mdogo wa refinery? Naomba elimu..
 
Zamani yote walikuwa wapi ,mbona sijaliskia Kwenye awamu ya viwanda
 
Border ya tunduma inavusha zaidi ya tankers 200 kwa siku na ukienda kwenye depot za mafuta Zambia kila siku unakuta hazija jaa.tazama depot inapokea mafuta kupita pipe line lakini bado tankers zinaendelea kushusha kila siku.biashara ya mafuta Zambia inapungua kipindi cha masika kwan migodi mingi inasimamisha uzalishaji.Zambia inapokea mafuta kutoka bandari Tatu,Dar port , Beira port na Walvis bay port namibia. Lakini haija wai kutokea depot zake zimeshindwa kupokea mzigo.

Back
Top Bottom