Bomoabomoa ya kibabe yatikisa Jiji

Jamani nimetingwa kidogo but I will come back on this sensitive topic niwape japo kidogo yanayotokea nchi za wenzetu hususan UK.
 

..dr,

..you don't sound like w.slaa!

..lakini, kama unavyowajua watanzania, wamebobea katika uvunjaji wa taratibu,kanuni na sheria. ziwazo zozote zile!

..umewaona wale waliojenga mabondeni, tena si mbali na hapo.

..umeona jinsi waswahili wanavyojenga hovyo hata kushindwa kuacha nafasi ya kupita mkokoteni.

..hata hivyo kosa liko pia kwa viongozi wetu, hasa pale wanapowaachia watu wavunje taratibu,kanuni na sheria, kwa maslahi yao ya kisiasa.

..na mengine mengi.
 

Dr Slaa

Mimi naamini misingi ya yote hayo ni kufanyia marekebisho au kuitunga upya kabisa sheria yetu ya arthi. Tumeona matatizo mengi yanarekeishika iwapo kunakuwa na malengo ya wazi ya namna ya kuyatatua. Suala hili la majengo holela ni suala la kimfumo wa sheria zetu zilivyo za kubahatisha kutemea ni nani amehongwa shs ngani au mjomba wake ana nafasi gani serikali.
 
Maisha Bora Kwa Kila Mtanzania.

Ari mpya
NGUvu mpya
KAsi mpya
 


Dar si Lamu

Naona maneno yako bado yanalenga katika kumlaumu Mwananchi. Dr Slaa kwa jinsi nilivyomsoma anatafuta mfumo mzuri zaidi wa kutatua haya matatizo. Mfano mzuri ni jinsi tatizo la ugonjwa wa malaria linavyoshughulikiwa; badala ya kuwalaumu wananchi kwa kutokufuata masharti bora ya kiafya...tumeangalia zaidi kwenye suala la elimu elimu na elimu na kwa kuongezea ugawaji wa nyandarua vyenye dawa bure...Zanzibar wamefakiwa sana kupiga vita malaria. Je tunaweza kufanya the same kwenye matatizo haya ya arthi? msukumo wa kitaifa utaolenga kuwaelimisha watanzania.
 

..yebo,

..hizo sheria,etc sio tatizo ingawa sisemi ziko sawa 100%.

..tatizo ni usimamizi wake! na zaidi uvivu katika kusimamia kazi na kutekeleza wajibu. hapa nawagusa wakuu wa miji na wapanga miji wao.
 


..the buck stops with mwananchi, and that's a fact.

..viongozi wanachaguliwa na nani?

..hao wananchi wangezikataa hizo vyandarua, kungetokea nini?

..nani kati yao asiyejua kutapisha choo wakati wa mvua ni kuamsha kipindupindu?
 
Hata kama ujengaji wa nyumba ulijengwa kwenye kiwanja ambacho ni rightful yours, hawa hawa wanaelewa kwamba hivi viwanja walivyojengea nyumba sio vyao/chako 100%. Tunajua kwamba serikali itapokuja kutaka kutumia eneo hilo kwa manufaa ya Umma, wanachukua anytime, sasa tatizo nini na waliombwa waondoke????
Mahakamani, kwenda kwao mahakamani pia haina maana wakishinda kesi wataendelea kukaa hapo; whether they win or lose kuondoka ni-inevitable! Sasa mlitaka mlipwe kwanza hizo nyongeza(kama mkishinda kesi) ndio mlete ma-uhaul kubeba mali zenu? Ulalamishi tu mmeonewa mmeonewa kila siku. Mmeonewa sasa nini hapa? WaBongo saa nyingine bwana…..!

Hakuna cha nchi za nje wala ndani kufanyaje vitu wakikumbwa na situation kama hii. Si kila kitu tuige nje bwana.
 
..the buck stops with mwananchi, and that's a fact.

..viongozi wanachaguliwa na nani?

..hao wananchi wangezikataa hizo vyandarua, kungetokea nini?

..nani kati yao asiyejua kutapisha choo wakati wa mvua ni kuamsha kipindupindu?


Mkuu

Haya unayoyasema yanaeleweka mijini. Tanzania ni kubwa sana, kuna sehemubado wanaamini kutiba malaria kwa uchawi au ni laana ya mizimu etc..elimu kwa wananchi na adhabu kali kwa watendaji ndio njia mbadala.
 
Mara kwa mara ninapata ugumu katika kuchangia mada ambazo zinatoa lawama upande mmoja na kuacha upande mwingine ukilemewa, wakati wote tunaelewa it takes two to tango.

Tatizo ni kwamba, falsafa yetu ndio imetufikisha hapa pamoja na utamaduni wetu ambao tumeurithi toka enzi. Utamaduni wetu wa undugu umetufanya tujenge dharau kwa utaratibu uliowekwa kisa tunajuana, au tumetoka sehemu moja, au tulisoma pamoja ama wakwe wa fulani ni wakwe wangu pia etc etc. Sheria zinapindishwa ili ku-accomodate hisia zetu za kufahamiana. Sasa kimbembe kimekuja baada ya watu kuja kutunyumbulishia kuwa yale tuliyokuwa tunayatenda katika undugu ni sawa na rushwa au ufisadi. Tumebaki kunyoosheana vidole kila pembe.

Kwa nini tusijifunze kuwa kila anayefanya maamuzi fulani awe tayari kwa consequences zake?? Kuna mahala DSM watu miaka ya 80 walilipwa fidia, wakauza nyumba zile bila kuambia wanunuzi kuwa ni eneo tarajiwa la kubomolewa (kumbuka hatuna utamaduni wa kusoma habari au kufuatilia mambo yanayotokea and we always live for the day). Wanunuzi hawa walipopata fununu hizo wakauza nyumba hizo kwa watu wengine na wengine wakaishi humo bila kujua kinachowafuata hadi habari zilipowafikia. Haya bomoabomoa ikapita watu wakalia na serikali hadi serikali ikatoa maeneo kwa ajili ya hawa watu tena bure. Kumbuka serikali inatumia tax payers money. they are using the same money that people work for to bail out other people.

Binafsi, imefika wakati Tanzania kuamua kufuata sheria na pia kuzisimamia hizo sheria. Pale ambapo mtu anataka kuleta mipangilio mengine inabidi kum-shut down na kuhakikisha sheria inafuatwa. Yote tunayozungumza leo yatapunguzwa kwa asilimia kubwa sana.

Wenye kununua viwanja wawe informed. Wenye kujenga nao wawe informed. Matatizo kama haya yataepukwa.

Siku hizi unakuta mtu anajenga Hotel katikati ya residential areas. Anaweka baa katika residential areas, wapi na wapi? Noise polution ndio usiseme........ yote haya sheria hazifuatwi. Mkuu wa mkoa akitoa agizo, watu wanaamua kui-politicize kisa anajuana na mkubwa mmoja au mkubwa ni mteja wake mzuri.

We need to uphold the rule of law........
 
Hii inanikumbusha unyama uliofanywa na makaburu kule Soweto.
 
Bomoa bomoa inaendana na sheria za ardhi na mipango miji, kwa Tz sheria za mipango miji na ardhi nyingi tumerithi toka kwa waingereza ambapo iwapo nyumba imejengwa pasipo kuwa na kibali notisi hutolewa kati ya siku tatu hadi ishirini na moja ikimtaka mjenzi aeleze kwa nini amejenga nyumba hiyo bila ruhusa na kwa nini nyumba hiyo isivunjwe.

Ipo mifano mingi ya bomoa bomoa na huu ulipwaji fidia. Kwa mfano nchini Malaysia, Baadhi ya watendaji wa idara ya ardhi walikuwa wanashirikiana na developer ili kujipatia utajili wa haraka, Watendaji hao utoa taarifa la eneo ambalo linatakiwa kuendelezwa kwa baadhi wa waendelezaji, na waendelezaji huvamia maeneo hayo, na inapofika wakati wa uendelezaji, hulipwa fedha nyingi na serikali. Fedha hizo ugawana na watendaji hao.

Matatizo huwakuta wale ambao wanaishi katika maeneo hayo, ambao wengi huwa ni vibarua wa ujenzi kwa hao madeveloper tena ni wageni nchini humo( wengi toka Indonesia). Hawa hawapati kitu, na wanaposhindwa kuhama katika muda uliopangwa, nyumba zao huchomwa moto. Hakuna kutumia kijiko, ni kuchoma moto nyumba zao ambazo nyingi ni za mbao nyepesi pasipo kujali mali iliyokuwamo ndani ya nyumba hizo.
 
DAR Si Lamu, jiweke katika soli yao.Umeomba ploti miaka nenda rudi unazungushwa tu, hatimaye baada ya muda mrefu, inapatikana unatakiwa ulipe shs 500,000 lakini mshahara wake wake wa mwezi kima cha chini kwa leo 100,000 hata usafiri tu wa Daladala hautoshi, tena bado hakuna miundo mbinu ya aina yeyote. Unafanya nini? Nimezungumza nao sana, nimefanya utafiti wa kina. Ninakosa majibu ndiyo maana wanajenga Bondeni, wanakubali kusombwa na maji, lakini angalau mtu akae na mke wake na watoto wake. Ni shida. Nawaza kwa mfano tungekuwa na mpango mkakati kama wenzetu, kungelikuwa na Estate Developers, na financial facility accessible kwa mwananchi wa kawaida payable over 50 to 60 years. Ninapenda kutafuta solution ya kudumu watu wetu. Tusipende kulaumu hakuna asiyependa kuishi kwa raha na familia yake. Shida inawasukuma hapo walipo. Kazi ya Serikali ni kutengeneza mazingira bora kwa kila mtu, as a duty si hisani. Ndiyo maana ninahoji kukimbilia bomoa bomoa kabla hatuja 'exhaust avenues zingine za kusaidia binadamu. Anayevunja Sheria kwa makusudi ashughulikiwe kwa mujibu wa Sheria, lakini "Generalization is a serious crime" katika kujenga hoja.Nadhani Experience ya wenzetu inahitajika, na hakuna aliyesema tu copy. But we do not have to re-invent the wheel either.
 
Naam sheria zinavunjwa kwa utawala mbovu ulio madarakani. Hawapimi viwanja na kuwauzia wananchi ili wajenge makazi yao, badala yake huko wizara ya ardhi kumejaa rushwa na ufisadi wa hali ya juu. Matokeo yake ndiyo hayo ya Watanzania kujenga hovyo hovyo. Sasa mnaenda kumvunjia nyumba mtu labda hana kazi hana biashara sikumpa huyu mtu na familia yake mateso ya hali ya juu. Ni kweli tunataka maendeleo, lakini maendeleo hayo yasifanywe katika hali ambayo inaawacha maelfu ya Watanzania kama siyo mamilioni katika hali ngumu zaidi kuliko waliyokuwa nayo kabla.


Mkazi wa Kurasini Zam Cargo, Joyce Mathias, akiwa amekaa katika eneo la wazi na familia yake wakati nyumba zikiendelea kuvunjwa kupisha upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam jumatano.Wakazi hao waliilalamikia Bandari kwa madai ya kutowalipa sehemu ya fedha wanazodai. (Picha na Yusuf Badi).
 

Mheshimiwa Slaa,

Sifikiri kuwa ni shida zinazowasukuma hawa watu kwenda kuishi katika sehemu zisizotakiwa. Shida zipo siku zote na ingekuwa ni shida basi wenye shida ndio wangekuwa wanakimbizana kila leo kwenda kusoma. Mimi nimewahi kuishi pembezoni mwa bonde la msimbazi, nyuma ya viwanda vya kipawa. enzi hizo bonde hilo lilikuwa jeupe na hakuna kilichokuwa kinafanyika ndani ya lile bonde. Tabata unaiona vizuri tokea upande wa pili na kwa wenye haraka, unatembea zako na kuvuka bonde tayari uko Tabata. Miaka yote nilikuwa napapenda sana lile bonde kwa ajili ya kwenda kujisomea. Nilikuwa natumwa kwenda kufua nguo bondeni, nilipomaliza kufua naankia pale bondeni nakaa chini ya mti na kujisomea na kufanya homework yangu. Baada ya mwaka hivi watu kutokea upande wa kipawa wakaanza kushuka kule chini kwenda kulima mashambaa ya mchicha hasa katika kipindi ambacho kilimo hicho kilikuwa kinawaingizia kipato kidogo. Basi kila mmoja aliyekuwa anaishi kule upande wa kipawa alijimegea shamba. Tena hakuna mwenyekiti wa kijij aliyeuliza. Badaye wenyeviti wakajifanya wajuaji na kuanza kubana watu huku na wao wakitaka sehemu kule chini.
Ndugu niliyeishi naye akahama kule na sikupatembelea kwa kipindi kidogo. To make the long story short, nilikaribishwa na rafiki yangu akiniambia tayari ana kiwanja maeneo ya 'tabata' basi nikaenda kumtembelea, alaa!!! Kumbe ni kule bbondeni nilipokuwa na fua nguo. Niliona nyumba zimeshamiri hakuna mfano, watu wanauziana viwanja kama njugu!

Haya utasema nini serikali ikiwa ilikaa kimya na kutokutambua maeneo ambayo wananchi wangeweza kuyavamia? Kulikuwa hakuna sheria?/

Ninachoweza kusema sisi watanzania ni 'opportunistic' in a sense. Tunapenda kutumia sheria pale zinapotunufaisha. Hawa watu waliojenga kule msimbazi hawakufuata sheria, kule kumejaa wapangaji wengi mno, wenye nyumba wengi pia. Kuna third generation of owners there as well!! Cha kuchekesha pia I was even offered a plot for 1.2Mil in that same area!!

Matokeo yake sasa naona watu wanaamua kufanya formalization of illegal procedures!! Ndio kuna wenye shida wengi kule, nilishahudhuria misiba ya watu kule bondeni na kila nikiwauliza why did you people chose to live here, majibu yao ni yaleyale, we had no choice!.

Come on!!! WE ALL HAVE THE CHOICE TO FOLLOW THE RULE OF LAW!! Tusihalalishe makosa yetu kutokana na shida zetu. Serikali ina sheria za ardhi, when people began migrating into Dar es salaam, the same people chose to look the other side, why?? Unakuta huyo mpima ardhi anafikiwa na ndugu ambaye hana uwezo wa kumtunza kwake basi akienda kutafuta eneo kule msimbazi anamwachia hapo. Kwake yeye amaesha-solve his problem but in the long run he has created a problem for the city.

Wafanyakazi wengi huwa wanajisahau they are part of the governement itself. we all are, tukibaki tunaimba serikali serikali, ni serikali ipi tunaongelea??
WE ARE THE GOVERNMENT![/I]
 
Tatizo la nchi yetu tunaishi kwanza ndipo tunapanga... tungekuwa tunapanga kwanza kabla ya kuishi haya yote yasingetokea. Watu wangejua (kabla ya Kujenga) kuwa hili eneo limetengwa na ramani ipo hatustahili kujenga.

Pili uwajibikaji wa maafisa ardhi nao ni wa mashaka. Kama watu hawakuuziwa wala kupewa viwanja hivyo naamini wasinge jenga na hata kama walijijengea kiholela bila kupewa wakati wanaanza ujenzi wahusika hawakuliona hilo ili wawazuie? ( Hapa ni sawa na vile vibanda vilivyobomolewa maeneo mbalimbali ikiwemo Posta Mpya- Ni wazi wakati vinaanza wahusika waliona na kuvifumbia macho sasa wana wanajidai eti watu wana makosa. Tukumbuke kuwa si wote tunaojua sheria na haki zetu kama watanzania, wengi bado tuna ile imani katika katiba kuwa kila mtu ana haki ya kuishi mahali popote ili mradi havunji sheria.... (sasa ni wangapi wanazijua hizo sheria kama hawafundishwi aukuelekezwa toka mwanzo?)

Mnadai wamelipwa fidia ... ni kiasi gani hicho? Na je kinalingana na maisha ya sasa hivi? Fidia hiyo imecalculatiwa kwa rate ya mwaka upi? Ule aliojengea nyumba yake au kwa sasa ili imwezeshe mvunjiwaji kujenga nyumba nyingine?... Nasikia kuna mama alisema kuwa wanalipwa 30,000 sijui kama nilielewa vema hapa. Nakumbuka Baba yangu alikuwa anatakiwa kuwa mmoja wao wa wahanga wa kuvunjiwa nyumba katika ule waliouita msitu wa hifadhi.. bahati yeye kidogo mambo ya ardhi anayajua aliwaonyesha risiti na hati zote kuwa amekipata kihalali baada ya kuuziwa na Ardhi na kama wanataka kuvunja basi wamlipe fidia kwa rate za mwaka huo waliokuwa wanataka kuvunja na si vinginevyo- walishindwa na mpaka leo anaishi pale.

Kusema kweli mimi naona kama hawa wanaadhibu mwenye haki--- ni sawa na mtoto aliyejisaidia sehemu ambayo baba anajua kabisa hairuhusiwi ila anamtizama kisha baadae anamwadhibu mtoto yule kwa kujisaidia pale... kwani baba wakati najisaidia hukuniona? kwa nini usinikataze hata kama ni kwa kiboko?

Haya ndio maisha bora kwa kila mtanzania??? hebu nijiendee zangu kuuona mwanga bora au kujumuika na marafiki wa kweli.
 

Pleaseeeee

hata kama nyumba zilijengwa kienyeji, ndio serikali imlipe mtu cheque ya shilingi elfu thelathini? (30,000)? sasa kwa 30,000 mtu akitoka hapo anaishi wapi? maana hata kodi ya chumba kimoja ya miezi sita uipati iwe sehemu yoyote ile dar

Kuondoka ilikuwa lazima lakini lazima shiria ifuatwe na haki ya binadamu itumike
 
.......... Mamlaka husika zilikuwa wapi wakati hao watu wanajenga?

.......... hawakuwa na ramani ta mipango miji? kwa nini unawaacha watu wanahamia sehemu ambayo unajua haitakiwi hausemi, unakaa kimywa ukisubiri uje kuwadhalilisha na kuwakomoa baadae?

watanzana wengi hatujui sheria, sasa kama wenye mamlaka ya kujua ninavunja sheria kwa kuishi sehemu nisiyotakiwa wanakaa kimya? huyu mtanzania ataota?

wahusika wafanye kazi zao sahihi, mfano kama huo ndio ninausubiri uje kutokea wakati siri kali itakapoamua kupanua barabara ya Old Bagamoyo, njia inayotoka kawe kutokea ubalozi wa marekani. watu wanajenga majumba makubwa tena sehemu ambazo ni hifadhi ya barabara, serikali na wahusika wa ardhi wanakaa kimywa wanasubiri kuja kuwavunjia wakati ukifika bila kujua hasara watakayoipata, kwa nini wasiwasimamishe sasa?
 
..yebo,

..hizo sheria,etc sio tatizo ingawa sisemi ziko sawa 100%.

..tatizo ni usimamizi wake! na zaidi uvivu katika kusimamia kazi na kutekeleza wajibu. hapa nawagusa wakuu wa miji na wapanga miji wao.


I agree with you Dar si Lamu

I'm sure kama watu wa mipango miji wangevalia njuga ujenzi holela kama wanavyovalia njuga bomoa bomoa tusingefika kote huku

solution ya kwanza kabisa kuzuia haya yasitokee tena ni kufuata mikakati yote iliyowekwa kuhusiana na ujenzi holela, then along the way serikali iboreshe zaidi mipango ya makazi

haileti maana kabisa wanaposema ujenzi holela hautakiwi hapa mjini halafu kila unapoenda kuna nyumba zinajengwa na misingi inachimbwa, kama raia wabishi kwa nini wasiite hao wanamgambo kuwabolea wakati wanajenga msingi? na wakitaka kutahadhalisha watu seriously inawezekana kabisa, mbona hatujawahi kuona mtu anajenga kwenye viwanja vya jeshi?
 
..yebo,

..hizo sheria,etc sio tatizo ingawa sisemi ziko sawa 100%.

..tatizo ni usimamizi wake! na zaidi uvivu katika kusimamia kazi na kutekeleza wajibu. hapa nawagusa wakuu wa miji na wapanga miji wao.


I agree with you Dar si Lamu

I'm sure kama watu wa mipango miji wangevalia njuga ujenzi holela kama wanavyovalia njuga bomoa bomoa tusingefika kote huku

solution ya kwanza kabisa kuzuia haya yasitokee tena ni kufuata mikakati yote iliyowekwa kuhusiana na ujenzi holela, then along the way serikali iboreshe zaidi mipango ya makazi

haileti maana kabisa wanaposema ujenzi holela hautakiwi hapa mjini halafu kila unapoenda kuna nyumba zinajengwa na misingi inachimbwa, kama raia wabishi kwa nini wasiite hao wanamgambo kuwabolea wakati wanajenga msingi? na wakitaka kutahadhalisha watu seriously inawezekana kabisa, mbona hatujawahi kuona mtu anajenga kwenye viwanja vya jeshi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…