Bomu lililotegwa Tehran miezi miwili iliyopita lilimuua Haniyeh

Bomu lililotegwa Tehran miezi miwili iliyopita lilimuua Haniyeh

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363

Bomu lililotegwa Tehran miezi miwili iliyopita” lilimuua Haniyeh - New York Times​

.

Chanzo cha picha,AFP
Maelezo ya picha, Ismail Haniyeh, mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas, akiwasili kushiriki katika hafla ya kuapishwa kwa Rais mpya wa Iran Masoud Pezeshkian katika bunge la Tehran Julai 30,
Saa 2 zilizopita

Katika mkusanyiko wa magazeti leo tumesoma ripoti inayozungumzia habari mpya inayohusiana na mbinu ya kumuuwa kiongozi wa Palestina Ismail Haniyeh na makala inayozungumzia athari za mauaji ya viongozi waliokuwa na uadui na Israel katika suala la mateka.

Tunaanza ziara yetu na gazeti la Marekani, The New York Times, ambalo waandishi wa habari walihitimisha kwamba mauaji ya Ismail Haniyeh, mkuu wa ofisi ya kisiasa ya harakati ya Hamas, yalitekelezwa na kilipuzi ambacho kilisafirishwa kwa siri hadi kwenye nyumba ya wageni ya Walinzi wa Mapinduzi ya Iran mjini Tehran yapata miezi miwili iliyopita.

Gazeti hilo la Marekani linasema kuwa lilitegemea maafisa saba kutoka Mashariki ya Kati wakiwemo Wairani wawili pamoja na afisa wa Marekani.

Watano kati yao walithibitisha kuwa bomu hilo lililipuliwa kwa mbali, baada ya kuthibitisha kuwa Haniyeh alikuwa chumbani mwake.

Maafisa wa Mashariki ya kati walisema Haniyeh alikaa katika nyumba hiyo ya wageni mara kadhaa wakati wa ziara yake mjini Tehran, na kwamba ingawa Israel haijakiri kuhusika na mauaji yake, mashirika yake ya kijasusi yaliifahamisha Marekani na serikali nyingine za Magharibi juu ya undani wa operesheni hiyo katika matokeo ya hivi karibuni, ilisema ripoti hiyo.

Uvumi uliokuwepo ulidai kuhusu uwezekano kwamba Israel ilimuua Haniyeh kwa shambulio la kombora kutoka kwa ndege isiyo na rubani, sawa na kombora lililorushwa kwenye kambi ya kijeshi huko Isfahan mwezi Aprili, ambalo lilizua utata wakati huo kuhusu pengo katika ulinzi wa anga wa Iran.

Gazeti hilo linasema katika makala yake - iliyoandikwa na wanahabari wake watatu - kwamba safari hii operesheni hiyo ilitumia mwanya tofauti wa usalama katika jengo la makazi ambalo lilipaswa kulindwa vikali, lakini liliruhusu bomu kufichwa kwa wiki kadhaa kabla ya kulipuliwa.

Gazeti la Marekani halikujua jinsi bomu hilo lilifichwa katika nyumba hiyo ya wageni, lakini maafisa wa Mashariki ya Kati waliozungumza na gazeti la New York Times walisema kwamba mauaji hayo yalichukua miezi kadhaa kupangwa na kuhitaji ufuatiliaji wa kina wa boma hilo.

Gazeti la Marekani halikujua jinsi bomu hilo lilifichwa katika nyumba hiyo ya wageni, lakini maafisa wa Mashariki ya Kati waliozungumza na gazeti la New York Times walisema kwamba mauaji hayo yalichukua miezi kadhaa kupangwa na kuhitaji ufuatiliaji wa kina wa boma hilo.

Maafisa hao wawili wa Iran walisema hawakujua jinsi au lini vilipuzi hivyo vilitegwa kwenye chumba hicho.

Gazeti la New York Times liliwanukuu maafisa wa Mashariki ya Kati liliozungumza nao wakisema kuwa mlipuko huo ulitokea saa 2 asubuhi kwa saa za huko, na kwamba wafanyakazi wa jengo hilo walikimbia kutafuta chanzo cha kelele hiyo kubwa, hadi walipofika kwenye chumba cha Haniyeh.

Timu ya madaktari katika jengo hilo ilikimbilia chumbani mara baada ya mlipuko, na kutangaza kwamba Haniyeh alikufa mara moja. Walijaribu pia kumfufua mlinzi, lakini pia alikufa.

Maafisa hao wawili wa Iran walisema kuwa kiongozi wa harakati ya Jihad ya Kiislamu ya Palestina, Ziad al-Nakhalah, alikuwa anakaa karibu, lakini chumba chake hakikuharibiwa sana, ikionyesha mipango makini katika kumlenga Haniyeh haswa, kwa mujibu wa makala hiyo.

Gazeti hilo la Marekani pia limesema, likiwanukuu maafisa wa Iran, kwamba usahihi na ustadi wa shambulio hilo ni sawa na mbinu ya silaha ya roboti yenye udhibiti wa mbali ambayo Israel ilitumia kumuua mwanasayansi mkuu wa nyuklia wa Iran, Mohsen Fakhrizadeh, mwaka 2020.

BBC
 
Bomu lililoua kiongozi mkuu wa Hamas lilitegwa miezi miwili kabla

Hiyo nyumba ikawa chini ya uangalizi wa majasusi wa Israel Mosad masaa 24 miezi yote

Majasusi walipokuwa na uhakika yupo ndani wakawasha remote kutokea mbali likalipuka likamuua yeye na Mlinzi wake

Jeshi la Iran hata hawajui hiyo remote ya kuwasha hilo bomu ilikuwa wapi na ilitokea upande upi

Source vyombo mbali mbali vya habari vya kimataifa


View: https://youtu.be/vVmFEfOQmc8?si=lfTm7EJFPcftoM9r
 
MOSSAD kaa nao mbali,ukiingia kwenye anga zao kamwe hutapona kabisa.Kutokana na gazeti la "The New York Times" inasemekana bomu hilo lilisafirishwa Kwa usiri mkubwa kutoka Israel mpaka Iran na kuliseti katika nyumba ya kulala wageni ambayo ndo alikuwa amefikia Ismail Haniyeh.Wakati bomu linakuja kulipuliwa Kwa remote control walihakikisha Kiongozi wa Hamas yumo ndani.
Havahana na MOSSAD.Ukiingia kwenye anga zao utakufa tu aijalishi ni muda gani watachukua kukuua.
 
iran wanatapatapa, wameshatoa tangazo leo tena kwamba wamegundua kuna projectile ilirushwa kutokea nje ya lile jengo. hata hawajui ilikuwakuwaje.
 
Back
Top Bottom