Bonah Kimoli Segerea imekushinda, miezi 4 sasa Kata ya Bonyokwa Kisiwani Mtaa wa Oysterbay hatuna maji

Bonah Kimoli Segerea imekushinda, miezi 4 sasa Kata ya Bonyokwa Kisiwani Mtaa wa Oysterbay hatuna maji

activist

Senior Member
Joined
Jan 3, 2014
Posts
180
Reaction score
281
Ni miezi 4 sasa kata ya Bonyokwa Kisiwani Mtaa wa Oysterbay wananchi hatujawahi kuona maji. Pamoja na juhudi za kuwasiliana na Mbunge wetu Bonah inaelekea mfupa huu umemshinda.

Mpaka tunajiuliza mbona kipindi cha Utawala wa Mwendazake shida ya maji ilishaisha?

Serikali ya CCM jitafakarini sana, hii haina afya kwa chama chenu kwa sababu matatizo ni mengi kama haya ya maji, umeme kupanda kwa mafuta na ni wazi viongozi wa CCM wameshindwa kutatua kero hizi kwa wananchi.
 
Ni miezi 4 sasa kata Ya Bonyokwa kisiwani mtaa wa oysterbay wananchi hatujawahi kuona maji. Pamoja na juhudi za kuwasiliana na mbungwe wetu Bonah Inaelekea mfupa huu umemshinda. Mpaka tunajiulixa mbona kipindi cha utawala wa mwendazake shida ya maji ilishaisha? Serikali ya CCM jitafakarini sana hii haina afya kwa chama chenu kwa sababu matatizo ni mengi kama haya ya maji, umeme kupanda kwa mafuta na ni wazi viongozi wa CCM wameshindwa kutatua kero hizi kwa wananchi.
Huu ni ukweli. Kipindi cha Magufuli huko bonyokwa maji yalikuwa yanatoka japo kwa dhamu mara mbili kwa wiki.

Magufuli alipofariki tu na maji yakakata miaka miwili sasa ni maajabu kuwahi kutoka Tanzania
 
Ni sekta ipi serikali inafanya vizuri?
 
Huu ni ukweli. Kipindi cha Magufuli huko bonyokwa maji yalikuwa yanatoka japo kwa dhamu mara mbili kwa wiki.

Magufuli alipofariki tu na maji yakakata miaka miwili sasa ni maajabu kuwahi kutoka Tanzania
Punguzeni kelele sisi wana CCM tunapendwa sana. Hayo maji si ukachote kwa jirani? Mbona vijijini wanatembea kilometa tatu kutafuata maji na hatuoni wakilalamika? Nyie watu wa Dar mna tatizo gani lakini?
 
Pole sana aisee kama bado unaamini hawa wahuni wapo kwa ajili ya wananchi.
 
Back
Top Bottom