Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Katika pitapita za kila siku mtaani, hivi karibuni nilikatiza maeneo ya Vingunguti pembezoni mwa Bonde la Mto Msimbazi na kukutana na hali ya hatari kwa afya. Kiukweli mambo si shwari katika eneo hili, hasa usalama wa afya kwa wakazi waliozunguka eneo hilo.
Kingo za mto huo zimegeuka kuwa dampo la taka za kila aina ambazo zinatoa harufu kali. Watu wanaingia katika taka hizo kutafuta vitu mbalimbali kwa lengo la kuuza ili kutumia tena, jambo linalozua maswali kuhusu athari zake kiafya.
Baada ya kusogea mbele zaidi, nilishuhudia kundi la watoto wadogo wakiendelea na michezo kwenye taka bila kujua hatari za kiafya zilizopo. Hali hii ni ya kusikitisha, hasa ukizingatia kuwa mazingira wanayochezea yanawafanya kuwa hatarini kwa magonjwa.
Hatari hii inaweza kubwa ikitokea magonjwa ya mripuko ukizingatia, Nje kidogo kuna lango kuu la kuingilia ndani ya machinjio ya Vingunguti, unapishana na watu wengi wa kila rika, wakijipatia mahitaji yao ya kitoweo.
Jitihada za haraka zinahitajika kuboresha mazingira kwa ustawi wa wakazi, hasa watoto, na ni muhimu kwa serikali na wadau kushirikiana kulinda afya za wakazi wa Vingunguti na maeneo ya jirani.