Bondia Abdallah Pazi 'Dullah Mbabe amesema kwa sasa anapumzika kupanda ulingoni

TEAM 666

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2017
Posts
4,399
Reaction score
8,594
Mbabe ametoa kauli hiyo kwenye mahojiano na Mwananchi Digital ikiwa ni siku moja baada ya kuchapwa na Tshimanga Kantompa wa DR Congo.

Bondia huyo namba mbili nchini kwenye uzani wa super middle amesema amelazimika kujipa muda wa kupumzika ili kujipanga upya.

"Mwakani ndio nafikiria nitarudi ulingoni, ila kwa sasa wacha nipumzike kwanza, nitulize akili, nijipange upya ili niwe na ujio mpya nitakaporejea tena ulingoni," amesema.
 
mwananchi_official_1633940745507.jpg
 
Ametoka kupigana october, mwaka umebakiza miezi miwili inamaana ndani ya hii miezi miwili alikuwa anataka apambane tena
Na zamu hii angeweza hata kufa, kwani hakufanya mazoezi kabisa, na ndio maana waligombana na kocha wake, kwani promota alimpigia kocha wake kuwa kuna pambano ameliandaa dulla anatakiwa kupigana kocha akamwambia atapiganaje wakati yupo tu chanika hafanyi hata mazoezi?

Kama vipi lipelekeni mbele, promota akasema haiwezekani na azam hawawezi kukubali, kocha akakataa, akaachana nao, kumbe huko dulla alisasaini na mkataba kabisa!!!na hicho alichokutana nacho ndio stahiki yake.
 
Na zamu hii angeweza hata kufa, kwani hakufanya mazoezi kabisa, na ndio maana waligombana na kocha wake, kwani promota alimpigia kocha...
Huyu Dullah Mbabe anafanana vitu vingi sana na yule marehemu Thomas Mashali. Yaani wana vipaji vya ngumi, huku wakiwa na uelewa mdogo vichwani mwao.

Bila shaka wana cha kujifunza kutoka kwa Hassan Mwakinyo.
 
Tuache masihara kidogo Kwanini Dulla anapigwa na huenda akapigwa sana siku zijazo Dulla alianza Ngumi mwanzoni mwa miaka ya 2000 Kosa analolifanya Dulla alivyopigana pambano lake la kwanza ndivyo hivyo hivyo anavyopigana hii leo

Kwanza anapigana kutafuta KO, pili anatumia nguvu kubwa round za kwanza, na mwisho kabisa hua hajilindi Dulla bado anaamini kuwa anazo nguvu za kumaliza pambano mapema na ndio maana huwa anavamia na kushambulia kwa nguvu Dulla hua anaamini kuwa yeye ni mvumilivu hata ukimpiga vipi hauumii wala hachoki

Masikini Mzaramo wetu amesahau kuwa sasa hivi nguvu mwilini mwake zimepungua sana hivyo hatakiwa kucheza kwa kutumia nguvu pekee bali na akili Dulla amesahau kuwa uwezo kuvumilia ngumi kwenye mwili wake umepungua hivyo akipigwa inaingia na anaumia.

Mfano juzi alipigwa akaanguka kutaka kudhihirisha kuwa hajaumia akaamka haraka haraka akiwa na mawenge akayumba sana hadi akatema udenda Sasa jiulize alikua na haraka ya nini wakati ana Sekunde 10 za kupumzika?

Na mwisho kabisa Dulla amesahau kuwa Boxing imebadilika, mabondia sasa hivi hawagombani bali wanapigana Wanatumia akili kupata ushindi rudia lile pambano la Tony Rashid na Mahlangu wa Afrika Kusini?

utanielewa Dulla anapaswa kucheza kwa akili, anatakiwa kujilinda na kucheza kupata point sio kumaliza Kwa sasa ukirudi ulingoni cheza kama Abdallah Pazi sio Dulla Ubabe hauna nafasi kwenye Boxing ya kisasa.
 
Tuache masihara kidogo Kwanini Dulla anapigwa na huenda akapigwa sana siku zijazo Dulla alianza Ngumi mwanzoni mwa miaka ya 2000 Kosa analolifanya Dulla alivyopigana pambano lake la kwanza ndivyo hivyo hivyo anavyopigana hii leo

Kwanza anapigana kutafuta KO, pili anatumia nguvu kubwa round za kwanza, na mwisho kabisa hua hajilindi Dulla bado anaamini kuwa anazo nguvu za kumaliza pambano mapema na ndio maana huwa anavamia na kushambulia kwa nguvu Dulla hua anaamini kuwa yeye ni mvumilivu hata ukimpiga vipi hauumii wala hachoki

Masikini Mzaramo wetu amesahau kuwa sasa hivi nguvu mwilini mwake zimepungua sana hivyo hatakiwa kucheza kwa kutumia nguvu pekee bali na akili Dulla amesahau kuwa uwezo kuvumilia ngumi kwenye mwili wake umepungua hivyo akipigwa inaingia na anaumia.

Mfano juzi alipigwa akaanguka kutaka kudhihirisha kuwa hajaumia akaamka haraka haraka akiwa na mawenge akayumba sana hadi akatema udenda Sasa jiulize alikua na haraka ya nini wakati ana Sekunde 10 za kupumzika???

Na mwisho kabisa Dulla amesahau kuwa Boxing imebadilika, mabondia sasa hivi hawagombani bali wanapigana Wanatumia akili kupata ushindi rudia lile pambano la Tony Rashid na Mahlangu wa Afrika Kusini?

utanielewa Dulla anapaswa kucheza kwa akili, anatakiwa kujilinda na kucheza kupata point sio kumaliza Kwa sasa ukirudi ulingoni cheza kama Abdallah Pazi sio Dulla Ubabe hauna nafasi kwenye Boxing ya kisasa.
"Too much running" alisikika muamuzi akimwambia msauzi...! [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mbabe ametoa kauli hiyo kwenye mahojiano na Mwananchi Digital ikiwa ni siku moja baada ya kuchapwa na Tshimanga Kantompa wa DR Congo.

Bondia huyo namba mbili nchini kwenye uzani wa super middle amesema amelazimika kujipa muda wa kupumzika ili kujipanga upya.

"Mwakani ndio nafikiria nitarudi ulingoni, ila kwa sasa wacha nipumzike kwanza, nitulize akili, nijipange upya ili niwe na ujio mpya nitakaporejea tena ulingoni," amesema.
Bora astafu kabisa.
 
Huyu Dullah Mbabe anafanana vitu vingi sana na yule marehemu Thomas Mashali. Yaani wana vipaji vya ngumi, huku wakiwa na uelewa mdogo vichwani mwao.

Bila shaka wana cha kujifunza kutoka kwa Hassan Mwakinyo.
Thomas Mashali kilichomponza ni uwizi, ukabaji na tamaa za kijinga.

Kafa kizembe sana.
 
Back
Top Bottom