Bondia afariki Dunia baada ya kupigwa ‘KO’

Shadow7

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2020
Posts
24,606
Reaction score
39,289
Mwanamasumbwi wa kike raia wa Mexico, Jeanette Zacarias Zapata amefariki dunia baada ya kupita siku tano tu tangu kupokea kipigo cha ‘KO’ ulingoni.


Jeanette Zacarias Zapata, 18 aliyefariki dunia

Zapata mwenye umri wa miaka 18, alipigwa ‘Knocked out’ raundi ya nne dhidi ya bondia Marie Pier Houle nakupelekea mwamuzi wa pambano hilo kulisimamisha na dada huyo tolewa ulingoni akiwa hoi hajitambui.



Pambano hilo la ‘professional’ lilifanyika nchini Canada siku ya Jumamosi lilishuhudiwa, Zapata akipigwa ngumi nyingi mwishoni mwa mno raundi ya nne pasipo kuweza kurudisha hata moja wala kujilinda.

Promota wa mchezo huo, Yvon Michel amesema kuwa Zapata alipofikishwa hospitali na ‘ambulance’ akapata ‘coma’ kabla ya kufariki majira ya 3:45 alasiri.
 
Sasa Mwakinyo leo ataua ama?
 
Daaah

Yaani kaenda na chuchu zake saa sita
[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…