Bondia Canelo Alvarez amchakaza Golovkin kwa pointi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607

Bondia Canelo Alvarez amefanikiwa kumpiga Gennady Golovkin katika pambano la uzito wa kati (Super-middleweight) lililofanyika Las Vegas, Marekani, asubuhi ya leo Septemba 18, 2022.

Ameshinda kwa pointi 116-112, 115-113, 115-113 ikiwa ni pambano la pili kwa Golovkin kupoteza katika maisha yake ya ngumi na yote akipoteza dhidi ya Canelo ambaye ametetea mikanda ya WBA (Super), WBC, IBF, WBO na The Ring.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…