Yeah ila alimpiga za macho Mike Tyson,Hata hivyo aliwaweka kwenye ramani ya dunia ya masumbwi watu wengi sana... Kiufupi aliwapa maisha๐ ๐ ๐ kwahiyo wacha aendelee kuvuta pumzi kwanza
Ungeliweka na historia yake ya kuzaliwa.Moja Kati ya mabondia mahili wa uzani wa juu kuwahi kutokea huwezi kumsahau George Foreman.
Jana siku ya ijumaa mwamba ametutoka, ulimwengu wa ngumi na Sisi tuliopata walau bahati ya kupanda ulingoni hakika hatutamsahau huyu mwamba.
Machache Tu kuhusu George ni bondia anaeminika kuwa na ngumi nzito Sana, Kwa Hili Joe Frazier analifahamu baada ya kuvuliwa ubingwa wa dunia ndani ya raundi mbili na kuanguka chini (knockdown) mara 6.
George ndie bondia Mzee kuliko wote wa uzito wa juu kuwahi kutwaa ubingwa wa dunia akiwa na miaka 46 akimvua ubingwa Michael Moore aliekuwa na miaka 26 wakati huo. Moore alikuwa ndio ametoka Tu kumvua ubingwa Evander holyfield.
Zaidi ya hayo George ni bondia pekee kurudi ulingoni baada ya kustaafu Kwa miaka 20 na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa dunia.
George alichukua medal ya dhahabu ya olympic akiwa amepigana mapambano 26 Tu tangu angie kwenye masumbwi.
Utakumbukwa daima.
"The Big George Foreman"
Yeah uko sahihi, Don alikua muhuni muhuni fulani hivi๐ ๐ ๐Yeah ila alimpiga za macho Mike Tyson,
Tyson angekuwa Bilionea akiwa chalii mdogo sana akiwa na Don
Sanaa...Ila Tyson huwa anamchana mpaka leoYeah uko sahihi, Don alikua muhuni muhuni fulani hivi๐ ๐ ๐
Na yeye kwa kipindi kile angepata hizo pesa zingeisha tu, Tyson alizitumia poa sana pesa alizozipata kwa jashoSanaa...Ila Tyson huwa anamchana mpaka leo
Narekebisha mambo mawili Tu kwenye post yako:Rumble in the jungle....
October 30, 1974 Zaire
Hili lilikua pambano lake dhidi ya Mohamed Ali...
Kule Zaire (DRC) jamaa alifanywa achukiwe sana maana Mohamed Ali aliwaambia wacongoman kua George Foreman ni mbeligiji hivo Ali atampiga ili kulipiza kisasi cha wabeligiji kuwatesa wacongoman kumbuka wabeligiji ndo walikua wanaitawala Kongo...
Siku ya pambano Mohamed Ali alikua na mashabiki rundo wote wakiimba Ali mpige mbeligiji huyo.. "Ali boma ye..."
Na kweli jamaa alikula kichapo kama kahaba aliyefumaniwa...View attachment 3279887
George Foreman aka the Big George alizaliwa huko Marshall Texas tarehe 10 Jan 1949 ni mmarekani mweusi.Ungeliweka na historia yake ya kuzaliwa.
Tujue mwaka na uraia, pia nini kimemsibu kupelekea kifo chake?