Bondia raia wa Urusi Maxim Dadashev ameaga dunia baada ya pambano lake na Subriel Matias kumsababishia majeraha makubwa ya ubongo.
Dadashev mwenye miaka 28, alishindwa kutembea mwenyewe baada ya pambano hilo ambalo mkufunzi wake Buddy McGirt alilazimisha lisimamishwe katika raundi ya 11 baada ya bondia huyo kupokea kichapo kikali bila majibu.
Kwa mujibu wa BBC. Pambano hilo lilipigwa Ijumaa wiki iliyopita. Na punde tu baada ya pambano Dadashev alikimbizwa hospitali.
Madaktari waligundua kuwa damu ilikuwa ikimvuja kwenye ubongo na kufanyiwa upasuaji wa haraka, lakini akafikwa na umauti jana Jumanne.
Shirikisho la ndondi la Urusi limesema tayari uchunguzi umeshafuguliwa juu ya mkasa huo.
Katibu Mkuu wa shirikisho hilo, Umar Kremlev amedai kuwa kulikuwa na “aina fulani ya uvunjwaji wa taratibu”, na kuongeza kuwa: “Tumempoteza Maxim Dadashev. Ilikuwa ni nyota yetu inayochipua.
“Tutaiunga mkono familia yake, ikiwemo kifedha. Tutakamilisha uchunguzi wa kuangalia mzaingira ya pambano, tunahitaji kujua ukweli wa kilichotokea.
“Hili linaweza kutokea kwenye mchezo wowote. Naamini kuna mapungufu ya kibinadamu yamechangia, kulikuwa na aina fulani ya uvunjwaji wa taratibu"
Dadashev ambaye alikuwa akifanya shughuli zake za masumbwi nchini Marekani alishinda mapambano yake yote 13 aliyoyacheza kabla.
Ijumaa alipambana na Matias kutoka Puerto Rico katika jimbo la Maryland ambapo alisukumiwa makonde mazito na kwa kasi kali.
Mkufunzi wa Dadashev, Bw McGirt alieleza baada ya pambano kuwa “alishindwa kumshawishi” kukubali kushindwa, lakini akaamua kurusha taulo ulingoni baada ya kuona “akipigwa zaidi za zaidi kwa makonde ya wazi kadri pambano lilivyokuwa likiendelea.”
=======
(CNN) Russian boxer Maxim Dadashev has died in a US hospital after his fight with Puerto Rico's Subriel Matias.
The fight was on Friday in Maryland. Dadashev was 28 years old.
"Top Rank is devastated to report that Maxim Dadashev passed away earlier this morning due to injuries sustained during last Friday's bout," Dadashev's promoter, Top Rank, said in a statement. "Maxim was a talented fighter inside the ring and a loving husband and father outside the ropes. Our thoughts and prayers are with his family and friends."
"Maxim was a terrific young man," added Top Rank founder and CEO Bob Arum. "We are all saddened and affected by his untimely death."
Dadashev and Matias fought at MGM National Harbor in Oxon Hill, Maryland on Friday night. The winner of the fight would've been the mandatory challenger to Josh Taylor for his title belt.
Dadashev's trainer Buddy McGirt stopped the fight after the 11th round.
Matias was dominating Dadashev and was ahead 109-100, 108-101 and 107-102 on the scorecards at the time of stoppage, according to ESPN's Dan Rafael. In reviewing footage from the fight, McGirt could be seen and heard pleading with Dadashev to stop the fight, noting he had taken a lot of hits.
Dadashev had to be helped out of the ring, and he started to vomit and lost consciousness before making it to the dressing room, ESPN reported. He was taken to UM Prince George's Hospital Center in Cheverly, Maryland where he underwent emergency brain surgery for a subdural hematoma, which is bleeding in the brain, the network said.
It added that Dadashev had to be placed into a medically induced coma after the operation in order to allow the brain swelling to subside.
"As you can imagine the news this morning has devastated us all," McGirt wrote in a message to CNN. "Out of respect for his family I will refrain from making any comment at this time other than to say Maxim was and always will be a phenomenal young man and boxer."
Dadashev originally hails from St. Petersburg, Russia but was based out of Oxnard, California. He had a professional boxing record of 13 wins and one loss, with 10 of his wins coming by knockout, according to Top Rank.
The Russian Boxing Federation has announced that they have opened an investigation into the matter.