Boran Jakutay
Senior Member
- Apr 8, 2023
- 110
- 259
Taarifa za hivi punde zinasema kwamba, Bondia Mtanzania, Ibrahim Najum, amefariki dunia leo Aprili 27, 2023 baada ya kukaa hospitali kwa takribani siku tatu akipatiwa matibabu.
Bondia huyo Aprili 24, 2023 alikimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, kufuatia mfadhaiko alioupata na kuanguka chini mara tu baada ya kumalizika kwa pambano lake dhidi ya Laurent Segu, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Katika pambano hilo, Segu kutoka Dodoma, alimshinda Najum wa Mbeya kwa pointi za majaji wote watatu; (Jaji 01 - 35-40, Jaji 02 - 35-40, Jaji 03 - 35-40).