Bondia Mtanzania afariki baada ya kupigwa

Boran Jakutay

Senior Member
Joined
Apr 8, 2023
Posts
110
Reaction score
259

Taarifa za hivi punde zinasema kwamba, Bondia Mtanzania, Ibrahim Najum, amefariki dunia leo Aprili 27, 2023 baada ya kukaa hospitali kwa takribani siku tatu akipatiwa matibabu.

Bondia huyo Aprili 24, 2023 alikimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, kufuatia mfadhaiko alioupata na kuanguka chini mara tu baada ya kumalizika kwa pambano lake dhidi ya Laurent Segu, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Katika pambano hilo, Segu kutoka Dodoma, alimshinda Najum wa Mbeya kwa pointi za majaji wote watatu; (Jaji 01 - 35-40, Jaji 02 - 35-40, Jaji 03 - 35-40).
 
But it's definitely not a murder, however, let his soul rest in peace. Amen.
 
Dah... pambano nililiangalia hili TBC1....mpinzani wake alipewa milioni moja na Mh.Mavunde km zawadi kutokana na ahadi aliyoahidi kwake.....huyu aliyeshinda alikuwa akilia kwa uchungu sana kwa kitendo Cha mpinzani wake kuanguka ghafla baada tu ya kengele ya mwisho.....Ampunzike kwa Amani.
 

Ni michezo kama mingine but comes with cost. Alieshinda ameonyesha ubinadamu kabisa, ningeshangaa kama angepotezea as if ni kuku kafa . RIP kwake
 
Asije kuwa alipigana huku yupo kwenye mfungo.. Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un
 
pole kwa familia ya wafiwa, zanzibar tulivyokata huu mzezo mkatuona wajinga si ndio
ila michezo yetu ya kuvua samaki kienyeji adi kuliwa na papa na kupanda juu ya minazi kudondoka kuvunja nyonga unaona fresh buda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…