Bondia Tony Rashid avuliwa ubingwa ABU, yadaiwa ulikuwa wa koneksheni

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Hii ndiyo taarifa mpya iliyosambazwa mitandaoni, ambako inadaiwa Rais wa ABU Haucine Hauichi amegundua kwamba alama zilizotangazwa na Majaji wa mchongo zilipigwa karata tatu, keusi kekundu.

Kwamba alizopaswa kupewa Sabelo Ngebinyana wa S. Africa akapewa Tony Rashid kwa njia ya Uzalendo.

ABU inamtambua Ngebinyana kuwa Mshindi.

My take: Wote waliohusika na mchongo huu waondolewe kwenye mchezo wa ngumi.
 
naunga mkono hoja 100%. Japo sipendi ngumi za kibongo.
 
Hata kidunda alipigwa na Katompa ila katompa akadhulumiwa , sasa dunia ya ngumi imetustukia , tumekwisha
Katompa alitandikwa na Kidunda Hadharani ila sifahamu wewe binafsi una shida gani na Kidunda. Umejaribu kuandika nyuzi kadhaa uki mdhihaki na kumshutumu Kidunda ila kitu ambacho Nina uhakika nacho Kwa Africa wapo mabondia wachache sana wenye uwezo wa ku mchallenge Kidunda.

Ndiye bondia ambaye akipanda ulingoni anatoa changamoto ya uhakika Kwa mpinzani wake na ni vigimu kumshinda.
 
Hivi kwanini wewe huwa upo upande wakutangaza mabaya tu ya watu hata kuyasema na mema yao huwa huwezi

Au una undugu na shetani maana kwako wewe binadamu wema ni Lissu na Mbowe ila wengine wana kasoro

Bondia akishinda unakuja kukosoa kuwa kapendelewa akipigwa unafurahi kweli kweli

Hizi ni roho za watu waliopigwa na maisha huwa wanatamani kila mtu awe na shida kama zao

Bado una wakati wa kubadili hiyo hali chuki humuua anaehifadhi.
 
Hata kidunda alipigwa na Katompa ila katompa akadhulumiwa , sasa dunia ya ngumi imetustukia , tumekwisha
Hili niliwaambia watu wakanibishia.

Na lile pambano lakwanza lililokatishwa, ilikua kumnusuru kidunda kwasababu moto ulionekana kumuwakia wazi wazi.

Akaenda kujiandaa, kurudi pambano lapili akagongwa ila matokeo yakaandaliwa kivyetuvyetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…