Bonge asipokula siku 2 anapungua, mimi mwembamba mbona nakula mboga 8 wiki nzima niko vile vile?

Michael Ngusa

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2014
Posts
1,637
Reaction score
463
Wandugu,

Natamani kunenepa. Nimechoka kutaniwa mkomao! Sasa nina rafiki yangu ambaye ni bonge, yeye asipokula siku 2 utamuona kabadilika kabisa...yaani kapungua ni hatari! mimi ni mwembamba, kwahyo inaenda vise versa...yaani nile healthy. Sasa huu mwezi wa pili, nakula mboga nane, vyakula vyote vizuri kwa gharama yoyote. Asubuhi supu la samaki na mbwembwe kibao..mchana ndo usiseme, Menu hunichukua almost elfu 8, lkn siongezeki. Mwingine akashauri eti nifanye mazoezi, sasa si mazoezi yanapunguza mwili? na mm sitaki nipungue zaidi ya hapa. Mwingine akasema nipunguze kugegedana..sasa wakuu...nisipogegeda, vizuri mle nyie tu sio? Nishaurini ndugu zangu.
 
Sasa kama mboga nane zote za majani utanenepa vipi ?
 

Cc watu wembamba kwanza tunakuwa hatuna hamu ya kula ww inakuaje unakula, kisamvu, mchina, spinach, mnavu, tembele, majani ya maboga, majani ya kunde, na majani ya mpera? Hamu unatoa wapi?
 
jf ni mahala pa ajabu sijawahi ona maishani mwangu yaani hii post na hivi vicomnt vichache vimemaliza mbavu zangu,ntarudi zikiongezeka,ila mkuu kuna usemi unasema cheka unenepe jaribu hiyo mbinu.
 

Utakuwa hauridhiki na una Roho ya korosho. Kama hapo unavyomuonea rafiki yako wivu kwa mwili wake.
Upate na dozi ya Dushe la kutosha unahitaji protein pia.
 

Tatizo wewe mchoyo mnafiki na unaroho mbaya.hata kama ukila na kunywa mafuta ya nguruwe haitasaidia kitu jaribu kujichunguza.



swissme
 
Sasa kama mboga nane zote za majani utanenepa vipi ?

Wajua anakula mboga zisizokuwa na lishe
pembeni kaweka ugali mnene...mchana ugali mnene na maharage
usiku ugali mnene...wewe utanenepa na nini..??

 
Kama mahusiano yako hayako vizuri sio mke tu ata wazazi ndugu uwezi nenepa wenzako vitambi kwa sababu ya furaha akila anaridhika
 
mmh oi ukipata dawa nishtue!
maana nimekula kitimoto hadi mafuta yake ila bado tu

Tanzania ianzishwe CHACHAWETA sasa
 
Siku zote kujenga huwa ni vigumu kuliko kubomoa..Jaribu na wewe kuacha kula uone kama unakonda au lah!.
 
ili unenepe lazima kichwa chako kisiwe na mzigo wa matatizo, kula vizuri,relax, lala angalau masaa nane kwa siku, pia watu wanene wankula mara kwa mara, kula asubuhi, mchana na jioni hakutakufikisha mahali, jifunze kula mara kwa mara. asubuhi chai, baada ya muda karanga, kikipita chakula mbele yako huachi, usiwe mvivu wa kula. utanenepa mpaka utajichukia
 
Unakula vibaya tu, bado hujapata misoc ya kueleweka.
Mimi nilikua mwembamba kinoma kiasi kwamba wenzangu walikuwa wakienda swimming inabidi nitafute sababu ili mradi tu nisiende kuvua shati.

Nilikua hivyo almost miaka sita, nilikua napiga supu na chapati, maandazi ya kutosha asubuhi, mchana na jioni nafuta misosi kibao ila it wasn't even healthy and it never worked, in short nilikua nachezea kilo kama 55 ukilinganisha na urefu wangu nilikua ka fimbo.

Kula chicken breasts za kutosha na nyama nyama nyingine tumia hata smartphone kutrace your progress kupima nutrients intake, kaa upange vizuri ratiba ya misosi, alafu fanya pia na mazoezi ili usipate kijitumbo au mafuta mafuta kibao kwenye mwili then subiri, usiwe na haraka, ku-gain kilo ni slow process. Siku hizi nakomaa kuzipunguza tu zisizidi wakaja kuniita kibonge.
 
Wasukuma wana kitu kinaitwa michembe,ukipiga hyo utanenepa kama pepekalee
 
Wandugu,

Natamani kunenepa. Nimechoka kutaniwa mkomao! Sasa nina rafiki yangu ambaye ni bonge, yeye asipokula siku 2 utamuona kabadilika kabisa...yaani kapungua ni hatari! mimi ni mwembamba, kwahyo inaenda vise versa...yaani nile healthy.

you have very high metabolism rate.

Kama ungekuwa unatapika baada ya kula ungekuwa na Bulimia.

Ongeza kula carbs zaidi, kula pasta, noodles, wali, ugali, mikate sana, yaani kula mikate na mafuta mengi, utaona tofauti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…