Bongo Dar es salaam, masahibu ya utapeli

1gb

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2013
Posts
2,199
Reaction score
2,859
Waziii....!!!
Wiii....?

Basi nilizoea kuskia kwa vijana wenza mjini Chuo kikuu.
Hii yote ni kwa sababu ya watu wa rika mseto wanavyo changa vizuri akili yao/zao kwa nia mbaya ya kutapeli wengine,ili mradi kujipatia kipato haba au rukuki ili mradi wapate riziki tasa ambayo haizai pasipo kutumia akili vyema.

Hebu nianze na sahibu lililonikuta mimi mwenyewe..
Na wewe utaleta masahibu yako ili kupitia masahibu haya,wengi wajifunze.

Saa 10:47 jioni.
Kariakoo.


Nikaskia nyuma yangu oya white..white..
Nikajifanya simsikii..ni tabia yangu nikiwa katikat ya umati wa watu..
Kama sijaenda na mtu yeyote city center niko peke yangu,huwaga sina shobo na mtu..sitakagi urafiki wa kuzoeana hovyohovyo city center.

Niilikuwa nimebeba furushi la mazaga mazaga rambo kubwa jeusi limejaa.
Nikawaida yangu kufanya hivyo kila baada ya miaka miwili nikianza maandalizi ya kusafiri kwenda bush.
Haikua mara ya kwanza kufanya hivyo,wala sikua mgeni k/koo mitaa mingi naijua,nikimalizaga kufanya mambo yangu sipotezagi muda,basi huondoka na kuelekea nyumbani.

Nikafanikiwa nikakusanya yakutosha ...hela ikawa imekata, wallet inasoma 10k hapo nawaza nikipanda daladala atleast ntabakia na 9600 ntafika nayo mbagala,Ntafanyia mambo mengine ya msingi.
NIMEPITA ROUND ABOUT
(Sasa ni MATAA)
Nipo upande wa kulia ukiwa unaelekea stand mwendokasi Gerezani.
(Zamani haikuepo mwendokasi)

Nikashikwa bega..oya tall
Vipi, cheki kazi hii mwanangu nipoze nina arosto kinyama,kitu og hakivunjiki cheki (ikakunjwa mpk ikakutana nusu kwa nusu)
Sikia white nipe buku ten tu,unajua dukani inauzwa 50000.
Yote haya aliyazungumza chini ya dk 1 huku nikiwa sijajibu hata salamu yake.
Nikaipenda,ilikuwa ni sandals ya ngozi moja matata inavutia sana..
Wakati natafakari akanambia
Sikia tall vua ujaribu..usiwaze ntakupozea tutaongea..
Moyoni nikajisemea hili teja ntalipa 5000 tu.
Maana tyr nilikuwa nishapenda
Akanipa kimoja
Nikajaribu sandal ika fit fresh kabisa,size yangu kabisa (42)

Teja:Kwaio unasemaje waiti kazi ndo hiyo hapo.
1gb
: Skia mm nna haraka km unauza kweli, 5000 iko hapa karibu.
Kama hauuzi mm nawahi daladala tusipotezeane muda.
Teja:Aargh waiti so po unaua mwanangu...

1gb:Poa endelea na biashara.
(Nikawa naondoka zangu)

Sijapiga hata hatua tatu...
Nikaitwa tena..

Teja:Waiti skia niongeze hata jero barida nini we uondoke nacho..
Nikamwambia poa nikatoa mia nne nilikuwa nayo masalia ya chenchi mfukoni..
Wakati natoa kumpa..
Akasema acha nikufungie kabisa.
Ilikuwa ni kitendo cha kurudisha mkono nyuma na kutoa mfuko(rambo)
Fasta akatumbukiza kitu akazonga zonga..
Nikampa 5400,
Akanipa fuko lenye sandal zangu mpya.
Tukaachana,Biashara ikafanyika.
Nimetembea hatu hazizidi 7 nikashika vizuri kwa nia ya kutomasa ule mfuko.
Mhhh...lahaulaaa nikastuka nikasema mbona kuna bonyea sory gani hii inabonyea,wakati sandal ilikuwa ngumu kiaina na imara.
Nika funua tu kidogo nikaona katika mfuko wa juu ndani yake tena kuna mfuko mwingine umekunjwa ndo wenye hzo sandal..
Nikafunua tena kwa kuchana kidogo.

Weeeeee niloona kitu kimepauka ni lijiatu sijui la mgambo au constebo wa miaka nenda rudi wa kipindi cha utawala ule wa Jk..
Aisee hata sikujitaabisha kusema nitaenda kucheki vzr home.
Macho yangu yalitosha kuamini kuwa nilichokiona sijakosea..nikalitupa hapo hapo jirani na mtaro.
Nikaishia kutukana ki moyomoyo nakusonya njia nzima hadi nakamata chuma kuelekea mbagala.
Ndio hivyo nikawa nimeibiwa.
Hata sikugeuka nyuma niangalie alikoelekea yule tapeli
Nilijua kesha tokomea kona kona huko na haitakuwa rhs mm kumpata.

Baada ya kusafiri Bush niliporudi Town,kama ada wengi wetu si haba,aghalabu hutembea kariakoo mara kadhaa kuchua akseshoriz.

5:13 asubuhi
Uhuru street hatua kma 7 nikamuona yule teja.
Aisee hali niliyomkuta nayo siku ile/kipindi kile (alichonifanyia uhuni) hajabadilika yuko vilevile.

Safari hii nilimuona
Mkononi kabeba simu kaweka kwa tumboni kama kaificha kwa shati
Daaah nikakumbuka 5400 yangu daaah nikasema ms€ng€ huyu anakula pesa za laana ndio maana hata shavu hapati

Nikaachana nae..
Nikaendelea na mpango wangu siku hyo..

Baada ya miezi kadhaa nikaja gundua trick aliyoniibia kizembe yule teja.

Ni kwamba wanachofanya wanakuwa wawili.
Mmoja anakuwa anatafuta mteja wa kumwibia na ndie anaeongea na mteja kupatana bei.

Mwingine anakuwa nyuma kwa pembeni kidgo anafuatilia mapatano yenu,akishaona umekaa line upo tyr kununua ana kuja chap chap kwa nyuma ya huyo mliepatana,
Anampa kwa nyuma viatu feki.
Wakati huo huo, huyo teja anapeleka mkono nyuma kama anatoa mfuko,anapotoa anapokea na viatu feki kwa huko nyuma vikiwa kwenye mfuko anaongeza na mfuko mwingine juu ya viatu hibyo feki kisha anakupa.
Haipiti hata dakika moja.
Ni kitendo cha haraka sana.
Huwezi gundua watagundua walio nyuma ya huyo teja.


Kutoka wakati huo hadi sasa sijaibiwa teeena, hua nashangaa mtu akisema kaibiwa...
Naishiaga kucheka tuu.

Huo ndo mkasa wangu ulionikuta Bongo chuo kikuu Dar es salaam,Campus ya Kariakoo.
Hostel Mbagala.

Karibuni.
 
Aseee sijawahi lizwa hapo tangu linaitwa jiji la makamba mpaka sasa jiji la makonda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…