Bongo kunakera!

Yo Yo

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2008
Posts
11,210
Reaction score
1,720
Khaa!! soma mwenyewe from Chemi Che-Mponda's blog
 
Low lives wapo kote, hata huku viwanjani tunakutana nao.Sema elimu na exposure vinasaidia kidogo.
 
Low lives wapo kote, hata huku viwanjani tunakutana nao.Sema elimu na exposure vinasaidia kidogo.
Hawa wamezidi basi wanashindwa kuweka kibao cha for whites only.Haya maduka ukiingia mzawa unaangaliwa kama mwizi na hasa hivi vidada vinakera sana.

Bongo kunakeraa ukitaka heshima

1:Kuwa na Kitambi

2:Ongea kingereza

3:Kuwa mweupe(white man)
 
Wengi wa watu wa namna hii wana inferiority complexes, i hear you. Unge demand kumwona manager
 
Customer care Bongoland ndiyo hiyo- hiyo amekerwa kwa Mr Price tu. Nenda maduka mengine ama ofisi zingine, ziwe za serikali ama za binafsi, kama umezoea 'majuu' utalia!
 
Nilishawai kwenda slipway nika order supu ilivyo fika nikagundua kulikua na inzi wawili kwenye supu, hasira zikanipanda kishenzi nikamwita muhudumu kumwambia kwamba kuna inzi kwenye supu, nikajibiwa "Nikusaidie kuwatoa???".....
 
Mr. Price Nguo ya 150,000 yaani zaidi ya Rand 1000 (tena ya kike) du labda bongo, lakini in SA sidhani kama kuna nguo ya bei hiyo kwa Mr Price
 
Mr. Price Nguo ya 150,000 yaani zaidi ya Rand 1000 (tena ya kike) du labda bongo, lakini in SA sidhani kama kuna nguo ya bei hiyo kwa Mr Price
Hawa wamekuja bongo kuchuma.
 
Mr. Price Nguo ya 150,000 yaani zaidi ya Rand 1000 (tena ya kike) du labda bongo, lakini in SA sidhani kama kuna nguo ya bei hiyo kwa Mr Price

Alikuwa na nguo zaidi ya moja zenye thamani ya shilingi 150,000, na siyo nguo moja.
 
Nilishawai kwenda slipway nika order supu ilivyo fika nikagundua kulikua na inzi wawili kwenye supu, hasira zikanipanda kishenzi nikamwita muhudumu kumwambia kwamba kuna inzi kwenye supu, nikajibiwa "Nikusaidie kuwatoa???".....

Ungewala tu babu...maana nasikia eti ni source nzuri sana ya protein....
 
Naomba na mimi nithibitishe kwamba si mtu huyu peke yake, bali watu wengine ambao nawafahamu pia walifanyiwa hivyo, muda umefika wachukuliwe hatua za kisheria!
 
Hii Mr. Price Bongo big deal wakati South ndo duka bovu kuliko yote la nguo!
 
Unajua tatizo letu nyumbani Tanzania ni umasikini wa fikra especially amongst ourselves. Tunadharauliana sisi kwa sisi..Utakuta mtu ameajiriwa dukani kwa mhindi au position mbovu mbovu ya u teller kwenye bank ya kigeni, basi ukienda kutafuta huduma, these people I call them "gate keepers" watakuangalia kwanza umevaa nini, au una usafiri gani, na vitu vingine kabla ya kudecide wakupe huduma au wakuletee nyodo. Uzuri wa hapa States ni kwamba competition ni kubwa na ukimfanyia mtu "wrong" ubaya utavuma kuliko pale utakapompa huduma nzuri.
Kama wafanyabiashara bongo wangekuwa na concept kwamba sio kila shopper ni lazima awe buyer...na wakawa train hao associates wao kuwa na lugha nzuri ili kuwa turn hao shoppers into buyers....biashara nyingi zingefika mbali sana lakini kwa mwendo huu...mmh inasikitisha.
 

Sasa kiburi chao wanakosa midola ya dada Chemi, lol. Na mbaya zaidi reputation inadondoka, wao wanaweza kuona kumkatalia huyu dada ni kumtoa nyodo kumbe yeye angeweza kuwaambia washkaji zake kuwa kuna duka zuri na kuzidisha market yao.

Kazi tunayo sana.
 
Bongo kunakera, yaliyonipa mwezio kwenye hilo supermarket usiseme. Nilikuwa likizoni nikaingia dukani, huku nikatoa kamera yangu nilitaka tu kuchukua mkanda short ili kuwaonyeza wenzetu huku waone pia bongo kumekucha maduka kama hayo yapo. Bwana wee!! kaniandama guard mmoja mikwara mpaka kwa meneja wa duka hilo,baada ya kulazimishwa kufuta mikanda yote kwenye handcam haikutosha,nusura karibu waninyanganye kamera , iliponea chupupu. Kwenye lango la kuingilia hakuna hata alama mmoja inayoonyesha usipige picha, u usiingie na mbwa au usitumie simu ya mkononi etc. Nilibaki kusononeka.Hiyo bongo yetu kunakera.
Zak.
 
Hii kadhia inanikumbusha siku moja nilikuwa nakwea pipa la madachi, sasa wale wabongo na njaa zao kwenye ukaguzi wa tiketi wanakuja na maswali meengi utadhani upo fuleni ya kuingia sijui mbinguni? Lakini niligundua kinachowasumbua ni kijiba cha roho tu hawana la ziada. Eti mtu unampa tiketi, anaigeuza geuza kama mtu anayeikagua noti halali, anaiangalia weee halafuu anakuuliza unaenda wapi? Huu si ndo ujinga ? Lakini akija 'mdhungu' anapita fastafasta..
 

One word they are "Gate keepers"
 
Ni kweli Bongo inakera. Jee ni nani wa kuibadili hali hii?. Wenzetu mliobahatika kufika nchi za wenzetu, na kuona mazuri, mkirudi Bongo tuisaidieni nchi yetu ili kwa pamoja tiubadilishe. Hawa wenzetu waliobahatika kupata kazi kwa wazungu, tena wale waliopata promotion toka kujiuza mabarabarani mpaka hivyo vijikazi kwa vyeti feki, ukimkuta kazini anakuona kama ..... Tena huyo dada wa hapo the price ana bahati maana ungemripoti kwa duty manager, kama ni kaburu kesho yake hana kazi. Kama ni Mbongo mbona chupi angevua!.
ya vyeti feki
 
Wakuu achaneni na hiyo ya ukaguzi wa tiketi na visa uwanja wa ndege ambayo huwa inanibughuzi kinoma, mimi nina experience na walinzi wa bank ya Barclays Arusha...mwaka jana nilikuwa A-town kwa ka likizo kafupi. Nikawa nataka ku withdraw ka pesa kadogo kutoka kwenye account yangu.nikaona ngoja nitumie ATM za Barclays Bank kwa sababu kuna mtu aliniambia wana charge fees ndogo. Bahati mbaya sana au nzuri sana...wakati ninaenda Bank nilikuwa nimeandama na mzungu volunteer wa PeaceCorp. Kwa nini walinzi wasinizuie kwenye gate..wamruhusu mzungu kwenda...hata baada ya kuwaambia kuwa mimi ndio ninayetaka kutumia huduma ya ATM...wakasema ATM zao zina charge fees kubwa kwa Tembo kadi kwa hiyo I am better off kwenda CRDB Clock Tower. Yaani walishakuwa na assumption kwamba I am a Tembo Card holder kwa sababu ni mbongo. Nikashindwa kuvumilia nikawaambia waniitie manager kama hawataki niende kutumia ATM, baada ya kuona hivyo wakaniachia niende, huku nyuma yule mzungu akaanza kupiga nao kiswahili akawaambia kuwa mimi ninaishi Marekani. Baada ya kumaliza haja yangu wakati narudi gateni...jamaa wakawa wananichangamkia kinoma...nikaona hawa washenzi tu. I was so pissed kidogo niandike barua kwenye mgmt ya hiyo bank.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…