Bongo Movie: Serikali yazuia Steps Kushusha bei za Filamu

Bongo Movie: Serikali yazuia Steps Kushusha bei za Filamu

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imepokea malalamiko kutoka kwa wasambazaji wa filamu kuhusu ushushwaji wa bei za filamu uliotangazwa na Kampuni ya Steps Entertainment.

Wizara imeyashughulikia malalamiko hayo na kuona kuwa bei iliyotangazwa na Kampuni ya Steps Entertainment si halisi na itasababisha tasnia ya filamu kudharauliwa na pia haina tija katika tasnia ya filamu.

Wizara inaiagiza kampuni ya Steps Entertainment kusitisha kuanza kuuza filamu hizo kwa bei ya Tshs. 1000 mpaka hapo muafaka utakapopatikana katika kikao kitakachofaninya kati ya Wizara ya Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo, Wizara ya Fedha na Wizara ya Viwanda na Biashara.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO.
 
Serikali acheni kuingilia biashara, mambo hayo yamepitwa na wakati muwache soko lijipange lenyewe, ushindani katika biashara ndiyo unampa unafuu mwananchi (mnunuzi).
 
Wananchi walio wengi ni wa kipato cha chini. Na wengi wanao nunua Movie za ku Burn (Feki) sikwamba wanapenda bali Ukakasi wa kipato nao unachangia. Gharama Kubwa yaweza Changia undelezwaji na ukuaji wa huduma za ku Burn CD za Movie(Feki)
 
Iivi Tanzania system ya uchumi ni command economy au capitalist au mixed
 
Na hii ndio main point ya Steps, kwamba wanadhibiti pirates.

Lakini wapinzani wa steps wanaipinga hii kwa kusema kua huwezi kushindana na Jambazi kwa wewe kujigeuza na kuishi kijambazi!!
 
haina shida wao wazuie bt sisi tunazipata huku mtaani kwa jero. Buku nyingi sana kwa hizi muvi.
 
Iivi Tanzania system ya uchumi ni command economy au capitalist au mixed

Hapo hakuna command mkuu.Pia inakubidi ufahamu kuwa hapo wizara imeingia kama mlezi na haijapanga bei bali imetengeneza mazngra ya kushauriana na wadau ili kuleta maelewano.VP KAMA EWURA,SUMATRA, SSRA, WASINGEKUWEPO UNGE-ENJOY?HATA USA HAIKO NAMNA UWAZAVYO, SERIKALI IPO KAMA REGULATOR BOSI.
 
Hayo yote unayoyataja yako kwa mujibu wa sheria sasa haya ndo tatizo ya serikali kuwa mifukoni mwa watu mbona kila siku tunalalamikia ada kupanda hovyo wanasema hakuna sheria ya wao kuingilia?
 
Hayo yote unayoyataja yako kwa mujibu wa sheria sasa haya ndo tatizo ya serikali kuwa mifukoni mwa watu mbona kila siku tunalalamikia ada kupanda hovyo wanasema hakuna sheria ya wao kuingilia?

Wanapofanya hivyo huo unakuwa ni uhuni.HUWEZI SEMA ETI HAIWEZI INGILIA KWA KIGEZO CHA SOKO HURIA.SERIKALI NDIYE MSIMAMIZI MKUU.MARA NYINGI WANAPOJITOA WANAKUWA NA MASLAI BINAFSI.
 
Wanapofanya hivyo huo unakuwa ni uhuni.HUWEZI SEMA ETI HAIWEZI INGILIA KWA KIGEZO CHA SOKO HURIA.SERIKALI NDIYE MSIMAMIZI MKUU.MARA NYINGI WANAPOJITOA WANAKUWA NA MASLAI BINAFSI.

Hata katika hili kama sio wanatumika na wale wapigakelele basi wanamaufaa binafsi katika bongo m!a!v!i
 
Tatizo sio Steps E. Tatizo kubwa la kiwanda cha filamu TZ, ni hao wadau(hasa) wasanii. Kila siku tunawashauri unganeni muanzishe Public Company ili muwe na mipango mikakati ya kuinua tasnia yenu. Hawataki kazi kutangaza Nia ya kugombea ubunge, historia ya tasnia ya filamu haijatengenezwa, historia ya siasa tayari imeshatengenezwa.
 
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imepokea malalamiko kutoka kwa wasambazaji wa filamu kuhusu ushushwaji wa bei za filamu uliotangazwa na Kampuni ya Steps Entertainment.

Wizara imeyashughulikia malalamiko hayo na kuona kuwa bei iliyotangazwa na Kampuni ya Steps Entertainment si halisi na itasababisha tasnia ya filamu kudharauliwa na pia haina tija katika tasnia ya filamu.

Wizara inaiagiza kampuni ya Steps Entertainment kusitisha kuanza kuuza filamu hizo kwa bei ya Tshs. 1000 mpaka hapo muafaka utakapopatikana katika kikao kitakachofaninya kati ya Wizara ya Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo, Wizara ya Fedha na Wizara ya Viwanda na Biashara.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO.

Ninakubaliana na Serikali kuchukua uamuzi huo, issue sio kushusha bei kwani hao wanopirate wanaweza kushusha bei chini ya hiyo ya Tsh 1000. Cha msingi ni Serikali kulinda kazi za wasanii ili wasanii wafaidike, serikali ifaidike na wasambazaji wafaidike. Tujiulize kama kazi ya msanii itauzwa tsh 1000 msanii atalipwa shs ngapi? itakuwa ndogo sana. Niliwahi kutembelea nchi kama Namibia kwa kweli huwezi kukuta kazi za wasanii zimemwagwa mtaani na zinauzwa kwa bei chee...Serikali iwe serious, ishirikiane na wasambazaji ili kudhibiti wizi wa kazi za wasanii...hizo sticker hazijasaidia sana kwani ni nnjia tu ya Serikali kupata mapato yao lakini hakuna ufuatiliaji kama kweli kila anayeuza kazi za wasanii ana hizo sticker kwenye kazi yake! Napendekeza ya kuwa kuwe na ufuatiliaji mkali wa kazi za wasanii na adhabu iwe kubwa kwa wale watakaoukutwa na kazi za bandia ikiwezekana wafungwe jela kuliko ilivyo hivi sasa....
 
Serikali acheni kuingilia biashara, mambo hayo yamepitwa na wakati muwache soko lijipange lenyewe, ushindani katika biashara ndiyo unampa unafuu mwananchi (mnunuzi).
Kwa hiyo wacheza filamu si wananchi... Basi sawaa..
 
mkutano (majadiliano) baina ya wasambazaji na serikali badala ya kushirikisha wadau wote wa sanaa za maigizo na filamu ni kiashiria kwamba watayarishaji na wasanii hawana lao zaidi ya kusubiri waambiwe cha kutekeleza. na kwa hali hii tutegemee kazi mbovu za sanaa na zisizo na kiwango cha ushindani ndani na nje ya nchi. kwani ilivyo (haya ni maoni yangu: baadhi ya watendaji wa idara za serikali wanajali sana matumbo yao kuliko taaluma husika. Kutawaliwa na tamaa kwa watendaji wa idara za serikali walio wengi (si wote) ndio sababu kuu ya kuporomoka uzalendo na umahiri. Je hili nalo mpaka watu waandamane? Wabunifu wa maana walishaacha kufanya kazi hizo na wanatazama na si miaka mingi mbele hakutakuwa na tamthilia za kitanzania katika vituo vya luninga vya nchi hii. Hiyo ndio hali halisi
 
Back
Top Bottom