Bongo Movie wanataka kufufuka?

Bongo Movie wanataka kufufuka?

Master Legendary

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2013
Posts
576
Reaction score
876
Kama Mataycoon wengine wanavyofufuka kwa kasi naona na Bongo Movie wameanza kutikisa Macho.

Ingawa wanasingizia kifo cha Kanumba ndiyo kimewamaliza ila kiuhalisia kilichowamaliza awali ni kukosa Dira na kupenda kudandia vitu vya Dezodezo wapate kipato tofauti na Marehemu aliyekuwa anafanya jitihada kwenye Movie na kufocus mambo makubwa kwenye Tasnia.

Hawa waliobaki wengi wamepoteza mwelekeo ndiyo maana wengine wanakusanywa tu kama mafungu ya nyanya na kupelekwa kwenye siasa pasipo kujua wanawagawa mashabiki wao.

Wengine nasikia walikuwa wanauzwa na kujiuza kwa Vigogo na wenye fedha hadi wauza unga na kugeuza Industry kuwa Centre ya Wadangaji,makahaba ma Makuwadi.

Kama mnafufuka fufukeni ila anzeni safari ya kurudi mlipotoka mkaendelee na njia ya yenu huko mlikoenda au kupelekwa mmeshapotea mbali sana.
 
Back
Top Bottom