Bongo Movie ya (MOSES).Imedhalilisha sana wanawake!!

Bongo Movie ya (MOSES).Imedhalilisha sana wanawake!!

Sizinga

Platinum Member
Joined
Oct 30, 2007
Posts
9,374
Reaction score
6,857
Nadhani ndio movie inayopigiwa promo sana hapa bongo kwa muda huu. Kwanza nimpongeze Kanumba, kaicheza vizuri.
Halafu kuna sura mpya mpya nyingi nadhani ananyayua vipaji. Wasanii akina swebe nilizani wamepotea lakini jamaa kawarudisha tena, hii safi.

Ile kashfa ya zecomedy kwamba Kanumba hajui Kiingereza ime-prove wrong!! Jamaa kasimama kwenye english, kozi aliyofanya naweza sema ni success!! Haumi maneno, yupo straight forward, Hongera!!

Nije kwenye point, Kiukweli hii movie jamaa kawadhalilisha mno wanawake, mwanzo mwisho!! Kwa maoni yangu hii movie haistahili kuonyeshwa kwenye jamii(public). Jamaa kaleta dharau, kebehi, majivuno, ubaguzi, ushenzi kwa wanadada, ufirauni, na anajifanya yupo much know kupita maelezo.

Wadada wamedhalilishwa kwa kuitwa kila aina ya majina, like rubbish, takataka, ******, kichwa cha kuku, washenzi, malaya na majina yote machafu unayoyajua. Jamaa kawashambulia mno wanadada kwenye hii movie, sijajua target ya hii movie ni nini!!

Cha kunisikitisha hadi mwisho wa movie jamaa kapata msichana aliyemweka mimba, na anasema hawezi kabisa kumpenda na dhamana yake ni kwa ajili ya mtoto aliye tumboni, na ukiangalia kisa cha yy kutopenda wanawake ni cha ovyo sana!! kwa jinsi alivyowakebehi na kile kisa chake ni completely different. Kisa ni cha kitoto mno hakina mashiko!!
Hii movie ikiachwa hivihivi bila taasisi flani za kijamii kuikemea nadhani inaweza kuzalisha watu wa dizaini ile ya kutowapenda,kutowaheshimu na kuwachukia wanawake daima. Women need to prove themselves correct by demolishing and eliminating the Movie MOSES!! They need to make huge strike against the movie. Haifai!!
 
jamani ni wengi wamesema ile movie imewadhalilisha sana wanawake lakini ukiwa makini na kuifatilia utagundua kwa nini kanumba alikuwa na tabia zile za kuwaona wanawake wote tabia zao zinafanana mwanza wa hiyo movie inaonyesha jinsi gani kanumba anawadhalilisha wanawake lakini ukiifuatilia kwa umakini zaidi utagundua nini kilichotokea kwa kanumba alipokuwa mdogo na unyama alioushuhudia kutoka kwa mama yake mzazi kwa kitu alichokifanya kwa baba yake mpaka kufikia hatua ya baba kupoteza uhai wake kwa unyama wa mwanamke aliomtendea ushauri wangu jaribuni kufuatilia kwa umakini sana juu ya hiyo move na mtapata picha halisi kwa nini kanumba aliwachukia wanawake,
 
Hebu tuambie kwanza ilikuwaje akawachukia wanawake kiasi hicho.manake tusije judge kumbe ni wewe binafsi ndo uko na perspective wrong juu ya iyo kitu.tupe hints wengine sie hatuna tv.
 
LKn Movie ni kuvaa uhusika flani ili kuionyesha jamii mabaya au mazuri yanayofanywa katika jamii. Kumshambulia Kanumba kwamba kadhalilisha wanawake kw akuwatukana na kuwa ita majina mabaya na kuwatukana ni vitu vinavyotokea daily kwenye jamii zetu kila siku tuna soma na kusikia kwenye redio mme kamchinja mkewe na watoto. Lengo hapo kuionyesha jamii dhalilisho ambalo wanawake wanalipata ktk mahusiano au ndoa! Nadnhani alipaswa apongezwe kwa kuvaa uhusika vizuri sababu imekukuna na kukubamba vilivyo, otherwise MESSAGE SENT!!
 
Hebu tuambie kwanza ilikuwaje akawachukia wanawake kiasi hicho.manake tusije judge kumbe ni wewe binafsi ndo uko na perspective wrong juu ya iyo kitu.tupe hints wengine sie hatuna tv.

Soma comment ya juu yako #8, na ndio maana nimesema kisa cha yy kuwadharau wanawake wote na level ya kuwadhalilisha haviendani...embu fikiria yule mshkaji(baba wa kanumba) anamfumania mkewe yupo kitandani na jibaba lingine, yule dada anaongea nyodo huku dogo kajificha nyuma ya mlango...ni kisa cha kitoto kwa mtu kufikia hatua ile kuwadharau wanawake kiasi hicho.

na kama wenyewe wanawake hawaoni tatizo then jamii yetu ni tatizo...otherwise wote tuna matatizo!! Ila mi binafsi naona imevuka mipaka!!
 
Soma comment ya juu yako #8, na ndio maana nimesema kisa cha yy kuwadharau wanawake wote na level ya kuwadhalilisha haviendani...embu fikiria yule mshkaji(baba wa kanumba) anamfumania mkewe yupo kitandani na jibaba lingine, yule dada anaongea nyodo huku dogo kajificha nyuma ya mlango...ni kisa cha kitoto kwa mtu kufikia hatua ile kuwadharau wanawake kiasi hicho.na kama wenyewe wanawake hawaoni tatizo then jamii yetu ni tatizo...otherwise wote tuna matatizo!! Ila mi binafsi naona imevuka mipaka!!
ndugu kanumba alikuwa sahii na cha msingi hapa na anti ezekia atoe movie inayodhalilisha wanaume
 
Nawashagaa watu wanaopima uwezo wa watu ma kwa makasa madogo madogo ya kilafudhi na kisarufi ya kingereza. Wa welsh na hata wa scotish wengi tu wanachapia kingereza sasa ije kuwa mtu wa Tanzania

Kanumba sio mwalimu wa lingusitic. Hata bado angeendelea kuchapia sana bado ni mugizaji. mzuri kwa level ya Tanzania.


Siku si nyingi tutaanza kupima uwezo wa wanariadha na wacheza mpira wetu kwa kingereza.
 
Wapi hujaelewa??nadhani itafute hiyo movie iangalie...then njoo na comments!! hapo nimebrief tu!!
kujaribu kumuelewesha dio ni sawasawa na kujaribu kumwelewesha mweyekiti kwamba chama sasa kimepoteza dira, aache tu wenzake wampokee lakini navomjua hata aelewi ye anadhani wenzake ndo magamba
 
Hajadhalilisha wanawake ila kawaambia ukweli wanawake
 
Unalalamika kwa Kanumba kuwadhalilisha wanawake kwenye movie! Na hawa wanaodhalilisha kiukweli kwenye maisha yetu ya kila siku unampango gani nao, mi naona kajaribu kuonyesha kinachoendelea huku kwenye jamii yetu. Hivi kweli katika maisha yako hujawahi kusikia mwanamke akitukanwa live kwamba ni malaya!? Hapa wanaume waambiane kama kweli alichokiigiza Kanumba kipo basi kiachwe.
 
Mtoa mada umenifanya niitafute hiyo muvi niiangalie,cjaona kama amemdhalilisha mwanamke coz mwisho wa siku ujumbe aliokusudia kuufikisha kauwasilisha vyema.Kama hii muvi kaitunga mwenyewe hajakopi sehem basi jamaa ni jiniaz
 
Mtoa mada umenifanya niitafute hiyo muvi niiangalie,cjaona kama amemdhalilisha mwanamke coz mwisho wa siku ujumbe aliokusudia kuufikisha kauwasilisha vyema.Kama hii muvi kaitunga mwenyewe hajakopi sehem basi jamaa ni jiniaz
sijaiona ila kama umeiona I think topic closed
 
mkuu inaonekana wewe ulifeli mtihani wa kiswahi ukiwa kidato cha nne,au hukusoma kabisa somo hilo,ina maana hujui maana ya fasihi?
 
Back
Top Bottom