BONGO MOVIES KWA KWELI MMETUCHOKA WATANZANIA

BONGO MOVIES KWA KWELI MMETUCHOKA WATANZANIA

Uta Uta

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2016
Posts
3,740
Reaction score
8,751
Habari wanajamvi?
Leo katika kuperuzi peruzi u-tube nikakutana na interview moja aliyofanyiwa msanii, muongozaji na muandaaji nguri wa kimataifa wa filamu za action Aston Barnabas aka Vanbrado aka Van Damme. Katika interview hiyo alikuwa anaelezea juu ya uandandaaji na bifu la msanii mwenzake aitwaye Neylish, kilichonishtua ni kwamba walikubaliana waandae movies kwa gharama ya Tsh 2,500,000.00/= yaani Tshs millioni mbili na laki tano na senti sifuri tu. Sasa mi nikashangaa sana na kuhisi hawa wasanii wametuchoka sisi watanzania na hawako serious kabisa. Milioni mbili unatengeneza filamu kabisa ambayo unategemea kuja kuliteka soko la filamu Tanzania, kwa kiasi hicho utafanya nini hasa cha kuwavutia watanzania wa rika tofauti, uelewa tofauti na kushindana na filamu kutoka nchi nyingine? pia hizo filamu zenu mna malengo ziangaliwe tu kwa mtogore, Nzasa, Kibudi, Kwakopa na Kwamfuga mbwa pekee si nje ya nchi?
Pili hiyo kazi ya u director, u producer mnaipata kwa vigezo gani? maana mtu anatoka na filamu moja leo kesho unasikia keshakuwa director, producer, location manager, costumes (sijui ndio kitu gani), nk.
La mwisho ambalo linakela zaidi unakuta wewe director mke wako au mchepuko wako co-director, mwanao location meneger, mdogo wako mpambaji, wifi yako sijui anafanya nini, sasa hao wote wanakuwa na utaalam wa hayo mambo au ndio ili mradi si wabongo hatujui viwango. Ushauri wa bure kama mna milioni mbili mbili basi kusanyikeni hata watu hamsini mpate milioni 100 ili muandae filamu zinazoeleweka na kumvutia kila mmoja.
Kwa uhondo zaidi sikiliza interview wewe mwenyewe hii hapa chini;

 
2014 kuna movie inaitwa avatar ndo ilishika no. 1 kwa kutengenezwa kwa gharama kubwa duniani (sikumbuki imetoka mwaka gani).
nkaenda kuangalia behind scene yake youtube lakini nilichokiona aiseee hapana.
 
2014 kuna movie inaitwa avatar ndo ilishika no. 1 kwa kutengenezwa kwa gharama kubwa duniani (sikumbuki imetoka mwaka gani).
nkaenda kuangalia behind scene yake youtube lakini nilichokiona aiseee hapana.
Lakini pia, kuna movie kibaozinatengenezwa "low budget"kwa viwango vyao, lakinimovie inakuja kuhit pia.

Bongo movie ina mapungufu mengi, menginiya kiufundi.

Mimi kuna movies huwa naangalia,nyingine hata si za Marekani, movie ina story ya kuvutia tu, haina mlipuko hata mmoja, haina kupigana risasi, haina magari kukimbizana, ni story tu.

Movies kamahizi Bongo watu wenye ubunifu wanaweza kuzitengeneza kwa gharamandogo tu (sijui kamahiyomilioni 2.5 inatosha hata kulipa camera crew tu, hata ukipewa kamera za bure).

Milioni 2.5 probably ni hela ndogo sana,ila,bongo hata watu wakipewa budget ya kutosha, sina uhakika kama kuna ubunifu unaotakiwa.
 
movie ina story ya kuvutia tu, haina mlipuko hata mmoja, haina kupigana risasi, haina magari kukimbizana, ni story tu.
Nadhani hizi ndizo muvi ambazo bongo inabidi wajikite nazo lakini wao wanataka action, polisi anakimbiza gari na kuikamata kirahisi hata bila kupasua side mirror, ubunifu ndi janga la taifa hata wakija na muvi za story basi watkuja na hizo hizo ambazo umeangalia wewe huko ila wao itakuwa kwa kiswahili tu, ila mavazi na location zitafanana sana na haswa mavazi
 
Nadhani hizi ndizo muvi ambazo bongo inabidi wajikite nazo lakini wao wanataka action, polisi anakimbiza gari na kuikamata kirahisi hata bila kupasua side mirror, ubunifu ndi janga la taifa hata wakija na muvi za story basi watkuja na hizo hizo ambazo umeangalia wewe huko ila wao itakuwa kwa kiswahili tu, ila mavazi na location zitafanana sana na haswa mavazi
Tumeshakariri kwamba movie iliiwe nzuri nilazima iwena action, milipuko, magarikukimbizana, risasi n.k.

Wakati hatuna bajeti walauzoefu na movies za hizo.

Na hapohapo,tunaweza kutoamovies za stories tu zamifarakanoya familia, matatizoya kazini, changamoto za jamii n.k ambazo hazihitaji milipuko, magarikugongana walabajeti kubwa sana.
 
Tanzania tuna makabila mengi tu ambyo historia zake zinafurahisha na hazihitaji mambo mengi sana, tuna vitabu vingi tu vina hadithi nzuri sana kwa mfano kuna kipindi fulani nilisoma kitabu kinaitwa "umelogwa au umetumwa" kilikuwa na hadithi nzuri na wala haitaji mambo mengi, kuna akina Ben Mtobwa nk wametunga vitabu vyenye hadithi nzuri au hawa wasanii wanashindwa kwenda hata TBC wakaomba ile michezo ya redio ya zamani wakaigiza ambayo ilikuwa mizuri ilipendwa na wengi na hata kwa mazingira ya sasa inakidhi ikiboreshwa kidogo
 
Back
Top Bottom