Bongo movies na sakata la maadili mabovu, kwanini serikali iko kimya ya suala hili jamani!

Down To Earth

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2011
Posts
21,940
Reaction score
16,643
habari wana jf,

kwa kuanza tu niseme kwamba tasnia ya sanaa ya maigizo hapa bongo, almaarufu kama bongo movie, imeshika kasi kwa umaarufu kwa kiwango fulani japo ina mapungufu ya ubora wake! bongo movie imefanikiwa kuwatoa vijana wengi sana wakike pamoja na kiume kimaisha! hivyo basi, naweza kusema kwamba, kwa kiasi fulani, bongo movie imeweza kupunguza tatizo la ajira hapa nchini Tanzania.

sasa cha kushangaza ni kwamba, washiriki wengi wa tasnia hii ambao ni mabinti, wamekuwa ni watovu wa nidhamu kupita kiasi kwa matendo yao yao kidhalilishaji na yasiyoendana na jamii husika ikiwemo kupiga picha za uchi pamoja na kutoka na waume za watu na kuvunja ndoa za waume za watu!

sasa kuhusu masuala haya, je basata iko kwa ajili ya nini endapo vitendo kama hivi bado vinafanyika ndani ya sanaa?

ukiangalia tasnia ya uigizaji katika nchi ya nigeria, serikali imefikia hatua ya kutoa ufadhili wa kifedha wa mpaka dola millioni 200 kwa ajili ya kuisapoti tasnia hiyo kwa vile tu imeonekana kuleta mafanikio katika nchi!

sasa je, kwa poor thinkers na money mongers hawa, wakipewa millioni mia mbili na serkali yetu itakuwaje jamani??

mi nadhani ifikie wakati wasanii wa bongo waende shule!! ukiangalia profile nyingi za wasanii wa nigeria kwa mfano osuofia (aliyeigiza katika movie maarufu ya osuofia in london, kwa mfano tu, yeye ana degree ya electrical engineering kama sijakosea, ramsey noah yeye binafsi ambition zake zilikuwa ni kuwa rubani, basi tu aliingia katika filamu kwa force ya watu fulani!)

wasanii wa bongo wa tasnia zoote na si bongo movie tu wanahitaji kubadilika,

itafuteni elimu ndugu zangu, msimwache aende zake, maana huyo ndiye mkombozi wenu!!!!!
 
Hawa wanahitaji ban ya maana. Wanaleta umarekani hapa. Hawajui kama hayo ma-filamu yao tunaangalia na madogo zetu?
 
Serikali iliyooza haiwezi kuondoa uozo uliojaa nchini. Hao vijana wa bongo movie wataserereka hivyo hivyo na maadili ya kishetani mpaka wafike huko wanakotaka kufika, baadhi yao wakitumiwa kuuza unga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…