hapo! Hapo! Hapooooooooo!!!!!!!!!!!!
Shabiki wa muziki wa Taarab, ambaye hakuweza kufahamika jina lake mapema akijirusha kwenye jukwaa la Jahazi huku akiwa ni mjamzito asiyeonekana kukihurumia kiumbe alichonacho tumboni kwa yale aliyokuwa akiyafanya jukwaani hapo
Mpakate mpaka chini!
Mkazi wa Chang'ombe Dar es Salaam, Elizabeth Richard (kushoto) akimdhibiti kijana aliyejitambulisha kwa jina la Baraka Johnson, mkazi wa Yombo, aliyedaiwa kujaribu kumtendea kitendo kichafu cha udhalilishaji wa kijinsia, wakiwa kwenye msongamano wa watu waliokuwa wakiingia kwenye Mkesha wa kuliombea Taifa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa Jijini usiku wa kuamkia jana. Kulia ni Ofisa usalama akijaribu kutoa msaada
Wakazi wa Dar es Salaam, wakiomba dua wakati wa mkesha wa kuliombea Taifa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, usiku wa kuamki January 1.
Source: ***********.com