huyo ndo nyerere aliyejenga viwanda vingi hapa nchini na wapumbavu wakaviua. aliyetujengea highest brotherhood in africa na leo watu wengine wanamwona hafai, aliyetufanya kujiamini na kutotegemea manyanyaso ya wazungu kwa muda mrefu, leo hii angalia mpaka wachina wajinga nao wanatugeuza koloni, aliyetufanya tuishi bila njaa, tuishi kijamaa kama ndugu. Angalia kenya uchumi juu yetu ndio ila unamilikiwa na wachache na wengi ni kutoka nje ya nchi yao, watu wanakufa kwa njaa na bila care yoyote (ubepari na ukabila). sie tuko chini kiuchumi ndiyo lakini tunaishi kwa furaha. Afande selle aliimba ni heri ugali na mlenda kwenye amani kuliko nyama choma vitani. Tungetakiwa kutumia amani kujenga uchumi imara kama yalivyokuwa matarajio ya mwalimu, bila amani hamna maana ya maendeleo. nenda afrika kusini kaone nchi nzuri ila kila siku watu wanakufa kwa highest crime, xhenophobia, no brotherhood, apartheid. think about it.