Bongo uaminifu na kuaminiana waislamu wako mbali sana

DeepPond

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2017
Posts
41,728
Reaction score
103,997
Binafsi Ni mkristo mkatoliki na Niko kwny biashara Zaid ya miaka 18 sasa

Ila kiukweli jamii ya waislamu hasa wa Zanzibar, somali au bara wale wazee wa swala 5 Ni waaminifu sijapata kuona.

1. Kuna msomali mmoja mwaka 2008 ile bado mchanga biashara, hanijui simjui ndo mara ya kwanza nanunua mzigo kwake, ila aliniamini akanikopesha mzigo wa pesa ndefu kwamba nikishauza ntamtumia pesa zake. Kweli nikamrejeshea kwa uaminifu na tunafanya biashara vizur Hadi leo. Hatujawai dhurumiana hata Senti.

2. Kuna mpemba mmoja ni nafanya nae biashara yuko nje ya nchi mwaka wa 4 huu, simjui hanijui, Zaid ya calls na chats kupitia wasap, nilitumiwa TU namba kupitia mtu baki, ila uwa namtumia pesa ananitumia mzigo na mizigo mingine ananikopesha. Tunafanya biashara Safi kwa upendo wa Hali ya juu utadhani mtu na ndugu Yake.

3. Kuna ustadh mmoja msambaa anamiliki mpesa matawi kibao Hapa k'koo mengine kibaha na mbezi . Ila matawi yote mengine yanayosoma till za jina lake, kaweka mashehe wenzie waliokutana na kufahamiana mskitini na wanayamiliki na kuendesha 100% ili kutunza familia zao. Ustadh yeye kabaki na matawi 2 tu anayoyamiliki 100%.

4. Kuna mfanyabiashara mwenzangu Ni mrangi wa dodoma ila Ni shehe swala 5. Yeye tangu nimjue hajawahi kukopa pesa ya riba benki yoyote Hapa nchini, kwake riba Ni haramu.
Akiwa na shida na pesa au mtaji umeyumba anaazima kwa mashehe wenzie uko mskitini na kurejesha Kama zilivyo.

5. Kuna mwislam mmoja mrangi Yuko Moro, nmemtumia sana kipind flan nafanya biashara ya nafaka. Huyu Tumejuana TU barabarani Tena kijiwe Cha draft, nikawa namtumia pesa ananikusanyia nafaka na kupakia kwny fuso na kunitumia dar. Ila mpaka naacha ile biashara, hajawahi nidhurumu hata Senti moja. Tuna maelewano mazur Hadi Leo.

6. Mwingine Ni shehe mmoja msomali agent binafs wa magari used yuko japan, ila ana wateja wengi Tanzania ,Zambia Hadi Uganda na Congo. Mteja analipia,gari inasafirishwa Hadi Uganda,Zambia kwa uaminifu mkubwa.
Anasifiwa Sana uaminifu kule kwny uzi wa magari used japan.

7. Mwingine Ni mpemba mmoja shehe anajiita Abdulwahid Yuko zanzibar anauza tv Toka Dubai, anasifiwa Sana kwa uaminifu kule Uzi wa wauza tv. Nami pia nishafanya nae biashara,hanijui simjui, Nikamtumia pesa ndefu akanitumia mzigo wangu Safi kabisa nikaupata Bila longolongo.

Mifano Ni mingi Sana,
Ila nikiri waislamu wako mbali Sana kwenye suala zima la uaminifu.

Nawasilisha[emoji1431]
 
Hii mada nlikuwa naijadili jana na jamaa yangu mmoja,alikuwa anatetea unachokisema mimi nilikuwa napinga.Wewe ni mkristo na muaminifu kwa mujibu wa maandishi yako,mimi ni mkristo na muaminifu kwa jinsi navyojijua.
 
Hii mada nlikuwa naijadili jana na jamaa yangu mmoja,alikuwa anatetea unachokisema mimi nilikuwa napinga.Wewe ni mkristo na muaminifu kwa mujibu wa maandishi yako,mimi ni mkristo na muaminifu kwa jinsi navyojijua.
Nmefanya biashara na wakristo wenzangu mauzauza nmeyaona mkuu tofauti na wenzetu mashehe
 
Sio kwamba ni waaminifu Ila wanajua Kuna gharama kubwa italipwa ukienda nje ya mstari.
Kila shekhe anajua madhara ya Albadri.
Baba la baba mzee Mohamed hawezi kupita na hela za mama lao Faiza la sivyo kesho ataanza kuokota makopo hapo gerezani
 
Sio kwamba ni waaminifu Ila wanajua Kuna gharama kubwa italipwa ukienda nje ya mstari.
Kila shekhe anajua madhara ya Albadri.
Baba la baba mzee Mohamed hawezi kupita na hela za mama lao Faiza la sivyo kesho ataanza kuokota makopo hapo gerezani
Hup mfano wake utazua taharuki humu[emoji1]
 
Sio kwamba ni waaminifu Ila wanajua Kuna gharama kubwa italipwa ukienda nje ya mstari.
Kila shekhe anajua madhara ya Albadri.
Baba la baba mzee Mohamed hawezi kupita na hela za mama lao Faiza la sivyo kesho ataanza kuokota makopo hapo gerezani
Uislamu unafundisha kua,unapomdhulumu mtu na mdhulumiwa akamshtakia Mungu,basi dua yake hua hairudishwi,inaenda moja kwa moja kwa muumba,haijalishi umemdhulumu Mwislamu mwenzako au mtu wa dini nyingine,dhulma ni dhulma tu,

Karma lazima itakurudia tu,hiyo ndio sababu,mtu aliyedhulumiwa wala hahitaji hiyo albadiri.
 
Wanaroga wale , yaani Wana option zote , ukiwapa Chao fresh , ukiwazurumu wanakutoa busha , jidanganye uwazurumu uone ,binafs nafanya nao kaz Sana Kwa vile mi na hulka ya uaminifu kiukweli wapo vzuri , Ila Wana defence kubwa tuuu endapo ukienda kinyume .....
 
Kwaiyo albadili huwa Ni story za kufikirika au vipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…