Bongomovie na Tafsiri kichaa!

Bongomovie na Tafsiri kichaa!

Naisujaki Lekangai

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
1,340
Reaction score
1,377
Napenda sana kuangalia movie za kitanzania na kuzifurahia ila kuna kitu kinanisikitisha mno. Kitu hicho ni tafsiri za kiswahili kwenda kiingereza.Wanaotafsiri sijui wanaokotwa wapi kwani wanatafsiri neno kwa neno badala ya maana.Hebu angalia hii mifano uelewe ninachosema.
1.Bongomovie: Sipendi kuogelea, naogopa kuzama. Tafsiri ya kibongomovie: I not to swim I fear to sink. Hapa huyo mfasiri wa bongomovie kaokotwa stendi ya ubungo.Tafsiri sahihi ni:I dont want to swim am afraid of drowning.
2.Hali ya hewa mbaya, ndege haitatua.
Mfasiri wa bongomovie:Condition of air is bad plane not park .Tafsiri sahihi:The weather is bad the plane will not land.
Mifano hii inatosha ila iko mingi sana baadhi hata wewe waifahamu.
Enyi wahusika wa bongomovie, mkihitaji mtu wa kutafsiri movie zenu nendeni idara za lugha za vyuo vya dar es salaam achaneni na mtindo wa kuokota watu stendi ya ubungo.Sidhani kama huduma ya kutafsiri ni ghali kiasi cha kushindwa kuwatumia wasomi wa lugha kwenye vyuo.
 
Back
Top Bottom