- Source #1
- View Source #1
Wakuu hili la kwamba BoniYai amesema Chadema inakufa na kujizika yenyewe ni ya kweli?
- Tunachokijua
- Boniface Jacob (Boni Yai) ni mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kanda ya Pwani lakini pia amewahi kuwa Meya wa Kinondoni.
Mara baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika Januari 21, 2025 ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, kumekuwapo taarifa potoshi zilizomhusisha Boniface Jacob kutokana na kuonekana kumuunga mkono aliyekuwa mgombea wa nafasi ya uenyekiti Freeman Mbowe wakati wa uchaguzi huo. Rejea hapa.
Kumekuwapo na Chapisho linalodaiwa kuchapishwa na Boniface Jacob kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X kuwa aliwahi kutahadharisha kupitia kamati kuu ya chama hicho kuhusu kuibagua Zanzibar kwenye rasilimali na shughuli za chama.
Je ni upi uhalisia wa chapisho hilo?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia maneno muhimu (Key Word Search) ulibaini kuwa taarifa hiyo ni ya kutengenezwa na haijachapishwa na Boniface kupitia ukurasa wake wa X.
Chapisho hilo limetengenezwa kwa kuwekewa taarifa ya Jambo TV iliyoripoti kuhusu aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar, Saidi Issa Mohammed na wenzake watatu kufungua kesi dhidi ya chama hicho wakidai kuwa katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za chama Zanzibar imekuwa ikitengwa. Chapisho la Jambo ambalo ni la kweli limeambatanishwa katika ujumbe uliotengenezwa na kuonekana kuwa umechapishwa na Boniface kupitia X, jambo ambalo si la kweli.