Mfanyabiashara na mwanasiasa Boniface Jacob maarufu Boni Yai na mwanaharakati Godlisten Malisa na baadhi ya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo wakiwa katika viwanja vya mahakama ya hakimu mkazi Kisutu leo Jumanne Julai 30, 2024 jijini Dar es Salaam.
Boniface mkazi wa Mbezi Msakuzi Dar es Salaam na Malisa mkazi wa Moshi mkoani Kilimanjaro wanakabiliwa na mashitaka matatu ya uchochezi katika kesi hiyo ya jinai namba 11805/2024, wanadaiwa kuchapisha taarifa za uongo katika mitandao ya kijamii kinyume na kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa Mtandao namba 14 ya mwaka 2015
Chanzo: Mwananchi
UPDATE
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imepanga Agosti 29, 2024 kuanza kusikiliza ushahidi wa kesi ya kuchapisha taarifa za uongo kwa lengo la kupotosha umma, inayomkabili meya wa zamani wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob (42) maarufu kama Boni Yai.
Mbali na Jacob, mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo ya jinai namba 11805/2024 ni Godlisten Malisa (38) ambaye ni ofisa afya na mkazi wa Moshi mkoani Kilimanjaro.
Jacob ambaye ni mkazi wa Mbezi Msakuzi na mwenzake Malisa wanakabiliwa na mashtaka matatu, huku mawili kati ya hayo yakikabili Jacob pekee.
Uamuzo huo umetolewa leo Jumanne Julai 30, 2024 na Hakimu Mkazi Mkuu, Ushindi Swallo baada ya washtakiwa hao kusomewa hoja za awali( PH).
Pia soma
- Mauaji ya Robert Mushi ndugu wa aliyekuwa Meya wa Ubungo Boniface Jacob polisi wanahusika?
- Kamanda Muliro: Malisa GJ, Boniface Jacob wakamatwe kwa tuhuma za kupotosha taarifa za kifo cha Robart Mushi
- Utata sakata la ndugu wa Boniface Jacob: Kupotea mpaka kukutwa mochwari ya polisi, Amana wapigilia msumari!
- Hatimaye Malissa na Boniface Jackob waachiwa kwa dhamana