mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,309
- 4,798
Nikiri kuna changamoto kwenye vyama vya siasa, mimi sipendi kuumauma maneno kwa sababu mimi kweli ni wakili, lakini mimi ni mwanasiasa ninavijua hivi vyama, vina changamoto kubwa, vinaumiza na kukatisha tamaa wananchi.
Ni vyama ambavyo kwa kweli havionekani kujiandaa hasa kuwa mbadala wa CCM, yaani hatuchukii nafasi tuliyonayo ya kuwa wabobevu kwenye upinzani lakini tunaonekana tunajiandaa kuwa wapinzani wa kudumu na kugaiwa neema ndogondogo kutoka CCM.
Kwa hiyo kimsingi ni kama vyama vingi vimekaa mkao wa kujiandaa kuwa mashabiki wa kuishangilia CCM inapoingia na kutoka, na kuingia na kutoka lakini wao ni kugawiwa tu mapato yatokanayo na mechi ambayo mechi hiyo ni uchaguzi, kwa hiyo mimi ninafikiri tunahitaji mtazamo mpya katika vyama hivi.