Bonite Arusha kuna tatizo gani ?

kenethedmund

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2011
Posts
347
Reaction score
89
Ni ukweli usiofichika kwa wafanyabiashara wa mjini? ili kuweza pata Fridge la Bonite inaweza chukua zaidi ya mwaka. Mara ya kwanza nilifikiri utani ila mimi binafsi nilijionea,

nilihitaji fridge ya bonite kwa ajili ya dukani kwangu, wakaniambia natakiwa kuwa na crate za soda kama 15 ambazo nilinunua na msimamizi wa bonite wa eneo akaja nakuthibitishwa kuwa zipo sawa. akachukua copy ya tin namba yangu na copy ya leseni yangu ya biashara chakushangaza mpaka sasa mwaka umepita lakini hakuna cha fridge.

Na unapompigia simu anakuambia nina dharura nashughulikia. ushauri wangu kwa Mzee Mengi kna kundi la watu linamuaribia biashara kumekuwepo na "too much organization politics" kwenye ofisi hiyo ambayo imeenza kumuharibia biashara.

Wanaharibu reputation ya Bonite Arusha kwa ujumla,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…