Book review: predictably irrational by dan ariely

asahnte Roulette kwa kufufua huu uzi. tuna vitabu vingi tungependa kushare na wenzetu. umetupa sababu:bump2:
 
Last edited by a moderator:
Ushauri wangu kwa wale wote wenye kupendwa kusoma vitabu vya kuhamasisha, tufahamu kitu kimoja kua hawa wanaoandika vitabu ni watu wenye fikra kubwa na muonekano mkubwa sn, Si unaona huyo kwanza ni professa hlf wa chuo kikubwa duniani MIT, kwahiyo uhamasishaji wake ni mkubwa, tunachotakiwa ni kuwa makini kwenye maamuzi yetu, hawa wanaandika kutokana na uzoefu wao na mazingira yao, sasa tusikurupuke na kuelewa vibaya. jamaa ni mtu anaependa kubisha sana bila utafiti ndio tabia yake, nilivokua mwaka wa kwanza, niliona documentary kua Saudia Arabia wanataka kujenga mjengo mrefu duniani mara mbili ya dubai itakua ni 1.6 kilometer, ukiwa kwenye pick ya hiyo mjengo unapaona north africa, akabisha sanaaaa, haiwezekani, nkamletea documentary na nakala pia mzungu kafanya tathmini bado akabisha, nkamwambia chukua taswira hii, miaka 700 nyuma unadhani watu walijua km tutakua na ndege dude linapaa angani limebeba watu au mtu kafufuka sasa hivi wa kale ukimwambia cha kwanza si lazima akatae, lkn wenye uwezo wao wa kufikiri ataona hamna kinachoshindikana ndo maana tukafika hapa. sasa tulipoingia mwaka wapili sijui nani kamshauri au kamshawishi asome vitabu vile vya Think Big, Poor dad Rich Dad na Get rich or die Trying. alivosoma hizo akanfata akasema mzee nimejifunza kitu hamna kinachoshindikana hapa duniani, kibaya zaidi vitabu vimemhamasisha kiasi kwamba kaona shule inamchelewesha ngoja azame mzigoni kupiga madili, akaacha chuo kabisa ati billgates ali drop njiani, sasa mkuu wewe huna mtaji, hua uwezo binafsi au kipaji, cheti chenyewe huna, unaishi bongo, kwanini usivumilie upate cheti halafu uingie mzigoni ili kama biashara zikibuma (kuna profit na loss) basi una cha kuanzia hata kwenye kuajiriwa. Na watu wengi wapo hivi nawajua aisee, kwahiyo tusihadaike, kila kitu kina muda wake, kuna muda wa shule, kuna muda wa mapenzi na kuna muda wa kutafuta, tunapoamua kuchanganya haya ndo tunapokosa yote. Nawakilisha.
 
Interesting kwa kweli

Tabu huwa ukijua vitu sana inakuwa majanga, unaweza ushindwe kununua vitu vya promosheni na vyenye dhana ya 'high quality'

Kwenye masoko kuwa wanasema, hizi zote ni njia za kumfanya mtu afeel value ya pesa yake.

 
asahnte Roulette kwa kufufua huu uzi. tuna vitabu vingi tungependa kushare na wenzetu. umetupa sababu:bump2:
Kwakweli sielewi hii review ilinipitaje. Kitabu kinaonekana ukianza huweki chini hadi umalize. As most of women I love these manipulatinve techniques. hehehe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…