Uchaguzi 2020 Bora CHADEMA mngesitisha uzinduzi wa kampeni kufuatilia hujuma za wagombea wenu kuenguliwa

Nani alikwambia serikali inaweza tishwa na kibaraka?,kinyago ichonge yenyewe halafu ikitishe
 
Both can go together!! Multitasking.. (Kupigania haki ya wagombea kurejeshwa kwenye kinyanganyiro + kampeni)

Ni sawa na kwamba mpo watu 18 mnakula sahani moja ya Ugani na kila mmoja na kibakuli chake cha mboga, sasa mgawaji anakisahu kibakuli chako cha mboga either kwa bahati mbaya ama makusudi - je utachukua uamuzi upi ulio sahihi? Ukizingatia wale wengine wanashaanza kupiga matonge tayari..
 

Weeeee! Unataka CHADEMA wasusie uchaguzi kama walivyosusia uchaguzi wa serikali za mitaaaaaa na kama Maalim Seif alivyosusia uchaguzi wa Urais na uwakilishi 2015??????? Itakuwa ni uenda wazimu! Wameenguliwa kwasababu ya kutokuwa makini au kutokuaminiana(dishonesty)!
 
Inabidi afanye kampeni na kuwaelewesha wafuasi wa CDM kwanza, kuhusu Tume. Baada ya wafuasi kuwaelewa ndio sasa mtaiambia tume tunataka wagombea wetu warudishwe. Hapo wafuasi watakuwa wameshawaelewa ata mkiwaambia tunaandamana kuelekea tume wataenda. Ngoja tumsikie leo ataongea nini juu wagombea waliokatwa
 
Umehitimisha uzi wako vema. Kususa kampeni siyo sahihi. Waendelee na kampeni wakiwaelimisha wananchi kuhusu uchafu huu wanaofanyiwa. Hili ndilo jukwaa pekee la kuelimisha raia haki yao ya kuchagua kiongozi wanayemtaka.
 
Kanuni mzitunge mwenyewe, mshindwe kuzifuata wenyewe, mkatwe harafu muanze kulaumiana wenyewe.
 
Ukoona mtu angangania kukuongoza jua ni mchawi.


kauli mbiu ya CCM "fitna kwetu mwiko"
 
Awali walisema kampeini zikianza ndipo Lissu atazungumizia Ilani ya chama chake na sera. Niliwauliza ana sera gani juu ya Uchumi na Usalama wa Tanzania. Walinijibu, nisiwe na haraka wakati wa ufunguzi wa kampeni, kila jibu la maswali yangu litapatikana. Nasubiri majibu hayo.
 
Sawa..... kwa kuwa ni demokrasia kutoa maoni hata wajinga tunawapa nafas..
Kwani Bwashehe wewe hujui, na unajifanya hamnazo? Kama ndio umepevuka karibuni, unamjua Mzee Mtei ni nani? Kama unamfahamu, basi meza, Ukweli ndio huo, utake usitake ndiyo hivyo.
 

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…