Bora huduma za afya ziwe bure kuliko elimu

Bora huduma za afya ziwe bure kuliko elimu

Pesanyingi

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2023
Posts
1,157
Reaction score
1,983
Serikali ni bora itowe huduma za afya bure kuliko elimu.

Fedha za elimu bure zihamishwe kwenye afya ili madawa na huduma kwa ujumla vipatikane kwa urahisi kwa kila raia.

Ukiwa na afya mgogoro hata hiyo elimu huwezi kuipata. Ada zirudishwe shule zote za serikali ila iwe kiasi kidogo sana na kila mwenye mtoto hadi kule vijijini aweze kupata elimu hiyo kwa gharama ndogo sana.

Iakini pendeza pia ni kupunguza matumizi ya magari ya bei ghali(V 8) posho mbali mbali watu wanazopokea ili fedha hizo ziende kwenye afya.

Ukitaka kujuwa umuhimi wa afya basi tembelea mahosipitalini.
 
Ni wazo zuri, linahitaji kuangaliwa.

Lakini kwenye haya maisha elimu ni muhimu sana. Fikiria mtoto mdogo leo ashindwe kupata elimu hata afya yake sidhani kama itakuwa sawa.

Elimu ndiyo njia pekee ya kuifunza jamii namna ya kujikinga na magonjwa mbalimbali. Kinga ni bora kuliko tiba. Tukibaki tu kutibu mzigo utakuwa mkubwa sana

Fikiria kuacha kutoa elimu kwa jamii juu ya namna ya kuepuka magonjwa ya moyo, magonjwa ya kuambukizwa, wagonjwa watakuwa wengi sana.

Hata kutoa chanjo kwa watoto nk huhitaji kwanza kutoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa hizo chanjo.

Hata wanaotibu wale wagonjwa wanaofika hospitalini hawaishii tu kutibu kwa kutoa dawa bali huwaelimisha pia juu ya namna ya kuepuka magonjwa yaliyowasibu. Mfano wanaopatikana na malaria hupewa dawa lakini pia huelimishwa juu ya kujikinga na malaria (matumizi ya chandarua, usafi wa mazingira nk).

Kwa hiyo elimu ni muhimu sana, kwani Kinga ni bora kuliko Tiba. Elimu, elimu, elimu, elimu, elimu ni silaha kuu.
 
Back
Top Bottom