Bora kufanya kazi kwenye kampuni ndogo inayolipa vizuri kuliko kampuni kubwa inayolipa vibaya

JUMONG

Senior Member
Joined
Sep 16, 2011
Posts
107
Reaction score
59
Wana JF hivi kipi ni bora zaidi kufanya kazi kwenye kampuni ndogo(Isiyojulikana) inayolipa vizuri au kufanya kazi kwenye kampuni kubwa(inayojulikana) inayolipa vibaya?Kuna jamaa yangu mmoja aliacha kazi Standard Chartered Bank ambapo alitoka mtupu akaenda kufanya kazi kwenye kampuni ndogo(isiyojulikana sana) kwa watu ila inamlipa vizuri na imemuwezesha kujenga, kununua gari pamoja na kuanzisha miradi mbalimbali.Je kijana alikuwa sahihi kufanya maamuzi magumu?
 
siyo hayo tu ndugu yangu...ukienda club usijali umevaa nini bali jali uko na nani( binti wa heshima kiasi gani namaanisha)
 
Wana JF hivi kipi ni bora zaidi kufanya kazi kwenye kampuni ndogo(Isiyojulikana) inayolipa vizuri au kufanya kazi kwenye kampuni kubwa(inayojulikana) inayolipa vibaya?Kuna jamaa yangu mmoja aliacha kazi Standard Chartered Bank ambapo alitoka mtupu akaenda kufanya kazi kwenye kampuni ndogo(isiyojulikana sana) kwa watu ila inamlipa vizuri na imemuwezesha kujenga, kununua gari pamoja na kuanzisha miradi mbalimbali.Je kijana alikuwa sahihi kufanya maamuzi magumu?

Mimi kwangu niachotafuta sio jina la kampuni:
1.Mshiko
2.Na kazi ni endelevu na siyo kampuni ya kitapeli?
 
Hivi tunafanya kazi ili tujenge jina? au tupate mshahara?
 
Kwenye kazi siku zote unaangalia maslahi Kaka pamoja na job security!!
Sio unafanya kazi kwenye kampuni kubwa, wakubwa wanatoka matumbo wewe unakonda!!
Hayo yatakuwa sio maisha!!
 
ubora wa kampuni kwa mfanyakazi ni uwezo wa kumsaidia kufikia matarajio yake kimaisha na kitaaluma.
 
Wana JF hivi kipi ni bora zaidi kufanya kazi kwenye kampuni ndogo(Isiyojulikana) inayolipa vizuri au kufanya kazi kwenye kampuni kubwa(inayojulikana) inayolipa vibaya?Kuna jamaa yangu mmoja aliacha kazi Standard Chartered Bank ambapo alitoka mtupu akaenda kufanya kazi kwenye kampuni ndogo(isiyojulikana sana) kwa watu ila inamlipa vizuri na imemuwezesha kujenga, kununua gari pamoja na kuanzisha miradi mbalimbali.Je kijana alikuwa sahihi kufanya maamuzi magumu?

Uamuzi mgumu uko wapi hapo mkuu? mimi naamini wengi wetu tunafanya kazi ili kuwa na uwezo wa kumudu mahitaji muhimu na sio kujulikana kwamba unafanya kazi kwenye kampuni kubwa!
 
Hivi tunafanya kazi ili tujenge jina? au tupate mshahara?

Unazifahamu ngazi tano za mahitaji ya mwanadamu? Kama huna hela kwanza unaanza kufanya kazi ili upate pesa ya kukidhi mahitaji yako ya msingi, hii ni ngazi ya kwanza! Kuna wengine ngazi hii wameshaivuka ila wengi wetu tupo katika ngazi hii
 
Uamuzi mgumu uko wapi hapo mkuu? mimi naamini wengi wetu tunafanya kazi ili kuwa na uwezo wa kumudu mahitaji muhimu na sio kujulikana kwamba unafanya kazi kwenye kampuni kubwa!

Siyo siri vijana wengi hupenda kufanya kazi kwenye makampuni yanayojulikana bila kujali maslahi na job security lakini at the end wanajuta, kuna rafiki yangu mmoja naye alikuwa na mtazamo huo lakini alikuja kushtuka baadaye akabadili uamuzi huku wenzake aliograduate nao wakiwa wameishafanya mambo makubwa kimaendeleo.
 
Kwenye kazi siku zote unaangalia maslahi Kaka pamoja na job security!!
Sio unafanya kazi kwenye kampuni kubwa, wakubwa wanatoka matumbo wewe unakonda!!
Hayo yatakuwa sio maisha!!

mkuu kuna jamaa yangu anafanya kazi maersk, anadai wakubwa wanachota mpaka 200m lakin wao wanachoambulia ni aibu hata kusema.
 
Bora uwe na genge linalokulipa laki mbili kuliko supermarket inayokupa elf hamsini...
 
nikweli kunarikapuni moja ra mafisadi wa kikanada rinajina ra kufa mtuu rakini nenda ukatinge uone bora ukauze genge arafu linauwa watingaji migongo acha watu tunakwesha chadema hoyeeee jiunge na chama la ukweli
 
Barrick Gold Mine sasa Africa Barrick Gold weziiiiiii
 
Back
Top Bottom