Bora ndege ianguke tu

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Ikiwa yapata nusu saa tokea kupaa kwake ndege moja iliyobeba abiria zaidi ya 200
..ikasikika sauti tokea kwa rubani ikisema "injini moja haifanyi kazi na iliyobaki haina nguvu kabisa ni wakati wa kufanya maombi kwani muda sio mrefu ndege hii inaanguka,tumieni nafasi hii kuombana msamaha ili mfike mbinguni salama."
Abiria wakaogopa sana na ukimya na hofu vikatawala
David na Grace walikuwa ni mojawapo ya abiria wa ndege ile..
Grace:mume wangu nisamehe aidan sio mwanao ni mtoto wa yule mlinzi,na hata kipindi umetekwa wakat umefuata pesa benki ilikuwa ni mpango wangu ili nipate pesa ya ada ya boyfriend wangu chuo kikuu.
David:wala usijali mamy,unisamehe pia kwa kuwa nishatembea na wadogo zako karibia wote kibaya zaidi yule mdogo angel ni mjamzito
.watu wakiwa wanaendelea kuombna msamaha ikasikika sauti ikisema
"Asante kwa maombi yenu hali ya ndege imetengamaa na tutafika salama"
Watu wote "aaaaahhhh si umesema inaanguka tunasema ndege lazima ianguke hiii haiwezekani,kama imeshindikana tunaiangusha wenyeweee
 
Tutaishije na aibu zetu?
 
Hapo kweli bora ndege ianguke tu hakuna namna
 
Hahaha.....ila kuna wengine makauzu, kuliko atoe siri bora afe
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ngoja niisubiri ikipita huku kwetu niitungue kuwasaidia hao abiria.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…