Bora nichukiwe na Wana Simba SC ila ukweli huu Mchungu uliochangia Kipigo Kitakatifu cha Mzulu na Mkaburu Kaizer Chiefs FC niuseme

Mm naomba nichambue goli la tatu Kati ya magoli manne ili nielezee nini maana ya ushapu na umakini katika soka. Angalia Mpira unatoka nje upande wa kulia mwa uwanja ambapo yupo kapombe, anachukua Mpira anachelewa kuchukua na kuurusha kinachotokea wachezaji wa kaiza chief wanakuja kukaba nafasi. Kwa hali hiyo tayari kashakosa kuwa shapu kuchukua Mpira na kuurusha kwa timu yake angali bado hawajabanwa Sasa kinachotokea anarusha Mpira kwa mwenzake ashabanwa hana nafasi Mpira unapokonywa watu wanatiririka kwenda golini. Mtailaumu beki sawa ila kosa linaweza kuanzia mbali mwishowe akaja kubeba lawama mabeki wa kati
 
Ukimaliza uchambuzi wa Simba ulete wa Yanga! Hao chiefs tunawangoja kwa mkapa pale tuwaonyeshe shughuli! Hilo la kupigwa ugenini sio geni, hamna mtu anatakaga afungwe kwao.
Hizi unazoongea ni ndoto za mchana, na kujifariji bt kiukweli safari ya simba kwa hya mashindano kwa mwaka huu ndio imefikia tamati jana. Tujipange kwa msimu ujao labda.
 
Ulikua wapi kuandika hata yote KABLA ya Jana?

Ulitegrmea Simba ishinde kila siku?

Wewe Ni mpuuzi unayedhani unajua sana
 
Nadhani sasa tunaona umuhimu wa kuwa na ligi inayoendeshwa kwa viwango vya kisasa, professional FA inayoratibu kwa weledi mpira kwa manufaa ya nchi nzima na siyo timu mbili za Kariakoo, kuvutia uwekezaji mkubwa kwenye vilabu, uwepo wa academy nzuri, viwango bora vya makocha kwa vilabu vyetu, tupunguze uswahili na siasa kwenye mpira.
 
Nitakosa fadhila kama sitakupa like.
 
Wale jamaa sikuzote walikua wakiomba wapangwe na Simba, na siku waliyo pata uhakika watakutana na Simba walishangilia Kama wamechukua kombe. Wao waliamini Simba ndio timu dhaifu kuliko zote zilizobaki.
 
Sawa mtopolo tumekusikia
 
KAMA SIMBA HAINA SIFA ZA KUCHEZA ZAIDI YA ROBO FAINALI YA CL, UTOPOLO MNAWEZA?
 
Tatizo la Simba ni ukabaji na kukosa umakini kipa na beki,
Kapombe anajijua ni mfupi ila anapenda kukaa mbele ya mshambuliaji na hayo magoli ya namna hiyo tumefungwa sana, wawa huwa haruki sidhani kama Simba wako makini kweli maana wawa ni mchezaji wa ligi za ndani, Mkude ni janga anarudia makosa yaleyale kwa ile miili yao Nyoni alifaa zaidi kucheza ile mechi.Dilunga sijui kawaloga nini Simba kwani anapewa nafasi mchango sifuri.
Kahata na Morison hii mechi iliwahusu na Mugalu alitakiwa atoke kwa kifupi kaizer chief waliwasoma sana Simba ndio maana waliwaacha wacheze wanavyotaka wanafanya counter attack
 
Hiyo number tatu Manara akikusikia atakuita takataka,yeye alisema Onyango bado mtoto mbichi ana miaka 27,sasa huo uzee kautolea wapi,nyie ndio mnamchokozaga Manara.

Vyombo vya habari hivi hivi juzi wachambuzi wameitwa takataka na Manara,kwa hiyo acha wawasifie kwani wakiwaponda Manara naye anawashambulia anaamini kwa kufanya hivyo analinda brand ya Simba.

Hiyo number 7 ya kikosi dhaifu nayo naisikia leo manake Manara anasema mnavikosi vitatu (aka kikosi kipana) vinaweza cheza mechi tatu tofauti ndani ya siku moja ,kimoja kinacheza mechi za kimataifa,cha pili kinacheza na Yanga kwa Mkapa na cha tatu kina cheza na Azam Chamanzi na mkashinda mechi tatu ndani ya siku moja.

Ila hiyo number 6 kweli ni tatizo unakuta timu weekend ina mechi ya kimataifa,katikati ya week ina VPL zote zinafanya Dar kwa Mkapa,anawaomba wahairishe mechi ya VPL kwa ajili ya mechi ya kimataifa.Huu ni ujinga TFF inabidi waachane nao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…