Bora nichukiwe na Wana Simba SC ila ukweli huu Mchungu uliochangia Kipigo Kitakatifu cha Mzulu na Mkaburu Kaizer Chiefs FC niuseme

Wale jamaa sikuzote walikua wakiomba wapangwe na Simba, na siku waliyo pata uhakika watakutana na Simba walishangilia Kama wamechukua kombe. Wao waliamini Simba ndio timu dhaifu kuliko zote zilizobaki.
Na huo ndiyo Ukweli mtupu japo wana Simba SC wote hatutakii Kuukubali Ndugu yangu.

Sijaumia Kufungwa zile Goli 4 ila nimeumia sana jinsi Kocha wao alivyokuwa akitucheka Benchini.
 
Simba hawakuieshimu Kaizer Chief, Wachezaji walikosa nidhamu kabisa uwanjani
Sifa za Kipumbavu sana na Kinafiki mno kutoka Magazeti Maalum ya Michezo nchini CHAMPIONI na Mwanaspoti zimetuponza na Kuchangia Kipigo kwani kiliwaaminisha Wachezaji wetu na kuwapa Viburi wakijiona wapo mbali Kiuwezo wakati hawajafikia huko ila wanajitahidi tu kutaka kufika huko.
 
Wana Simba SC tuliaminishwa Kipumbavu kuwa Kaizer Chiefs FC katika Ligi Kuu yao bora barani Afrika ya PSL wako nafasi ya 9 na huku Kwetu Ligi Kuu yetu ya VPL TFF Magumashi Simba SC ni ya 1.

Jana walituzidi mno Kiufundi kila eneo.
 
Nakukubalia sana kwa hili 100% Ndugu.
 
Na huo ndiyo Ukweli mtupu japo wana Simba SC wote hatutakii Kuukubali Ndugu yangu.

Sijaumia Kufungwa zile Goli 4 ila nimeumia sana jinsi Kocha wao alivyokuwa akitucheka Benchini.
Kweli I see..niliumia Sana pale matola alionekana anatetemeka..na kocha wao alitucheka Sana kwa dharau Sana..dah!
 
Kweli I see..niliumia Sana pale matola alionekana anatetemeka..na kocha wao alitucheka Sana kwa dharau Sana..dah!
Kicheko kile kwa ninavyowajua Wazungu ( tena wakiwa Afrika Kusini / wakitokea Afrika Kusini ) pale alikuwa akitucheka Kidharau vile na hata Kututukana Moyoni kwa Upumbavu wetu wa kutokujua Mpira zaidi ya Kuubahatisha tu.
 
Furaha yangu kuona ndugu zangu simba wanateseka 🤣🤣
 
Nakubiliana na wewe %100.... Simba kiukweli jana wamezingua sanaaa na mpira waliocheza jana kama tukikutana na utopolo wakacheza ivyo tunauzwa vbaya sana
 
Me sio shabiki wa simba ,,ila kinachonisikitisha n pale linapokuja suala la timu kufungwa,,,watu mnaibua hoja ambazo upande mwingne hazna mantiki,,,kwani kipindi simba wanamaliza group stage kwa kuruhusu goli mbili ,,,umri wa hawa mabaki ulikuwa ni tofaut na wajanaa???

Nakubaliana na wewe kwamba ,,,kwanza simba walii underrate kaizachiefs kutokana na mwenendo wao kwenye ligi na jinsi wao(simba) walivyomaliza group stage,,,

pia suala jingne ndugu zetu straiker hawana zaidi ya mawinga na viongo wazuri..
Sijakupinga nimeongezea kulingana na uewelewa wanguu
Am out!!!!!!
 
Wakuu Kuna Kitu Kinaitwa Football administrators Hawa Ndio wanatakiwa kuwa waongoza njia, wananchama, mashabiki na wapenzi wa mpira wataelewa ikiwa wataona kuna maslahi mapana kwa familia nzima ya mpira.

Hizo ligi kubwa tunazozitamani haziongozwi na malaika ila watu wakipewa kuongoza ligi na FAs wanaweka pembeni unazi wa vilabu vyao, wanatumikia mpira kwa maslahi mapana.

Sisi hapa ni tofauti. Ukiwa nazi wa Yanga au Simba na ukafanikiwa kuwa kiongozi wa mpira unataka FA na ligi iwe kama tawi la timu yako.

Haiwezekani tukaendelea kwa mtindo huu. Ukumbuke kuwa 90% ya michezo yako unacheza hapa kwenye ligi ya ndani. Kimbembe ukienda kwenye CECAFA/CAF championships.

Kama una ligi na mfumo bora wa mpira utakuwa mshindani mzuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…