Bora shule ama kazi?

Changamka

Senior Member
Joined
Sep 27, 2015
Posts
149
Reaction score
161
Habari za Jumapili,

Sera ya nchi tunaambiwa "HAPA KAZI TU"

Mimi ni kibarua katika kampuni moja hivi ya simu za mikononi lakini mnajua maana ya kibarua unaweza ukaamka ukaambiwa "your no longer" huna kazi! Hakuna mkataba wa kudumu.

Na pia nina ada kabisa ya ya kulipia chuo college diploma miaka yote 3. Je nipige shule chini nibaki na kazi pamoja na biashara niwekeze katika
kununua mazao niweke ndani maana mwezi wa kwanza na wa pili nipige bao la maana?

Sijawahi kuona sera inayosema shule shule kwanza.


Fursa2017
 
Humu utapewa vitu vya kukuchanganya akili.

Unatakiwa kukaa na kuamua moja, Hili ni ishu personer na inadepend na levo ya Sprit ulio nayo.

Only Spirt ndo itakayo kuongoza.

Fanya maamuzi mwenyewe kwa kujiangalia mwenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shule ni safety net

Inakusaidia usife kwa stress ukiwaza huna plan B
 
Shule unataka ya nini?, kama unataka ikupe hela nenda kama ni fahari tu kalime maana hata kazi nyingine haitakufaa itakuboa.
 
Awamu hii siyo yakuacha kazi mkuu ikiwezekana soma night mchana nenda kazini

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha uoga...huu ndio wakati sahihi wa kuacha kazi hasa kama umeajiriwa...

by the way sijajua mtoa mada anasoma shule gani..nadhani ni bachelor degree...

ingekua masters programme angeweza kusoma huku anafanya ajira ila bachelor nashauri uache kazi ukasome ukimaliza njoo tujiajiri mtaani.

maana hata ajira zenyewe hazilipi watu kila siku wanalia njaa na kuishi kwa hofu ya kutumbuliwa...WATUMWA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maisha hayana formula.
Ila mtu aliyesoma maisha kutabirika ni rahisi sana kuliko mwenye shule zero.
 
Awamu hii siyo yakuacha kazi mkuu ikiwezekana soma night mchana nenda kazini

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahaa ndo mnavyo Danganyana?
Hivi kati ya Wafanya biashara na Wafanyakazi ni wapi wenye Maumivu?

Wafanyakzi wana hari mbaya usione watu wanaenda kazini nenda Huko Mahalimashauri uone mziki wa Magu ulivyo.

By the ways asikudanganye mtu na usidanganye mtu kwamba kazi ndo ina maisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hebu mwambie mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ukitaka kujua shule haina maana watu wote waliofanya ugunduzi wa mambo mbalimbali duniani ni watu ambao hawakwenda shule au waliachia njiani.
 
Kivipi? Ma profesa wasingekuwa wanalilia kuanza kufundisha kwa mkataba baada ya kustafu

Sent using Jamii Forums mobile app


Unadhania kuna profesa maskini!? Ukimuona profesa maskini nakuhakikishia atakuwa ni kilaza aliyebebwa hadi kufikia hatua hiyo ya uprofesa.

Ukiona wanahitaji kuendelea na kazi ni kwa sababu ya saikolojia yao kujengeka kwa kukaaa maeneo ya vyuoni na siyo kitu kingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…