Malenja jr
Member
- Jul 24, 2022
- 8
- 5
Katika mazingira ya kawaida tunayoishi katika jamii yetu Kuna dhana ambayo imejengeka kila kizazi kujiona bora kuliko kizazi kingine hapa nazungumzia kizazi Cha zamani kinachoishi mpaka Sasa na hiki Cha Sasa ambacho kinajiita Cha kidigitali.
Kizazi Cha zama za nyuma kinajivunia kwa kusema kuwa kulikua kuwa bora Sana kuliko Cha Sasa kikimaanisha kulikuwa kikifanya Mambo kwa ustadi mkubwa na kukubalika zaidi.
Kinaenda mbali zaidi kwa kusema nyakati zao elimu ilikuwa bora,utafutaji wa maisha ilikuwa bora hakuna aliekimbia majukumu Kama sasa,hata katika swala la mapenzi wao walioa wanawake vigoli na sio Sasa Hali ni mbaya.
Mzee mmoja ambae alijulikana kwa jina la Bitolo alianzisha maada hii katika kijiwe Cha kahawa kwa kusema kuwa "Vijana w a Sasa hamna kitu kabisa hawako Kama enzi zetu ndio maana sahizi wanapata taabu katika kila kitu Songombingo ni katika hayo mahusiano ya mapenzi" Mzee Bitolo alianza hivyo.
Wadau katika kahawa walichangia Ila walijikita zaidi katika swala la uwajibikaji na majukumu kwa kusema yafutayo.
1. Kizazi Cha Sasa ni wavivu, Zamani kijana wa kijijini ili uonekane sio mvivu ilikuwa nikuchapa kazi shamba hapo jamii nzima ilikuwa inamuona kijana huyo ni balaa na anafaa hata kuoa kabisa.
2. Ulimwengu wa sayansi na Techinologia, katika hili walisema kuwa Vijana wengi wamekimbilia mjini wameenda kutafta lakini ni asilimia chache Sana wanaofanikiwa kimaisha wengi wanarudi patupu wanakuja kuanza upya Tena na wengine wanaona aibu kurudi wanabaki kutumikishwa tu kule kwa ujira kidogo.
Katika Hilo niliunga mkono maana hata Mimi nilikuwa mhanga wa kisanga hiki Cha ujira mdogo Sana usiofaa mjini na kwa kawaida ni kweli Vijana wengi wanavumilia hili swala huko mjini.
3.Mahusiano ya Sasa "Mapenzi" kwenye maada hii ilionekana kuwagusa Sana Vijana na walisikiliza kwa makini nikiwemo na Mimi kupata madini ya nyuma kuhusu mahusiano ampapo mzee Bitolo alisema yaani zamani sisi familia yako inakutafutia mwanamke wa kuoa akiwa mbichii tukacheka ..hahahahaha.
Akaendelea kwa kusema Wengi sahizi watoto wakike wanazwlishwa hata bila ndoa Sasa hapo utalinganisha na sisi? Eti mtu anaelewa mwezi tu kashindwa sijui mna nini nyinyi Vijana wa Sasa.
Yaani kwa kifupi ni Bora Sisi kuliko nyinyi kizazi chenu ni Cha Kama Vipi,Vipi tu mnapenda kazi rahisi mno ndio maana mnakimbilia mjini hamna maana kabisa alimalizia hivyo.
Kijana mmoja akabidi ajibu mashambulizi Sasa kwa mzee yule na wale waliokuwa wakimuunga mkono mzee Bitolo
Mzee sio kwamba kizazi hiki nikivivu hapana inatakiwa mkubali tu zama zimebadilika sio Kama zamani.
Sizani Kama kizazi chenu kilikutana na hii tekinologia iliyopo kwa Sasa ni kwamba watu wanabadilika kulingana na mahitaji ya wakati huo.
Hatukatai kuwa katika vitu vingi tupo tofauti na kipindi chenu lakini kwa Sasa vitu vingi vimeongezeka na watu wanahitaji ndio maana kundi kubwa la Vijana wanaoneka wavivu na kupenda vitu rahisi.
Si kwamba ni rahisi kihivyo mkipewa mvifanye nyinyi pia hamuwezi kuvifanya.
Zamani ilikuwa rahisi kumtambua kijana asie na fedha ilikuwa anaonekana kwa mavazi yake tu wakacheka hahshahhaha.
Siku hizi Vijana wanapendeza na unaweza jua wanakipato hivyo ni ngumu kumtofautisha ni mpaka uongee nae akwambie bayana kifupi ni kwamba
"Vijana wa Sasa wamechagua kuwa na Tabasamu hata pale ambapo wanahisi Wana magumu" kijana alimaliza kwa kusema hivyo.
Naweza kusema kuwa nyakati ni tofauti Sana hivyo hakuna kizazi Cha kulaumiwa zaidi ya kuyachukua Yale mazuri yakizazi kile yatumike kuelimisha kizazi hiki ni dhahiri kinafanya mabaya lakini mengi ni mazuri ndio maana jamii zinaendelea ni vitu vya kimila tu ndo vinapotea ukilinganisha na Sasa.
Katika zana ya kawaida kabisa ni kwamba uwajibikaji wa Sasa na zama zile ni tofauti kijana wa Sasa anapitia changamoto nyingi mno katika makuzi yake hivyo inapelekea kuwa fikira tofauti hata katika uwajibikaji ,Mfano kijana anahitimu elimu yake ya chuo wengi wanawaza kupata ajira ya serikali lakini kwasasa nikipengele kikubwa Sana kuajiliwa serikalini.
Ni tofauti na kipindi Cha nyuma ndio maana Vijana wengi Sasa baada ya masomo yao wanajaribu kutafuta njia rahisi ya kupata vipato ndio hapo wanajikuta wanadondokea katika ajira binafisi maeneo mengi ni wanyonyaji katika ujira mdogo hivyo kijana atapata chakula na makazi ili aendelee kuwepo mjini.
Hii inatokana na aibu kwamba nikirudi nyumbani watanionaje,natakiwa kufanya kitu nyumbani Sasa mawazo haya yanawafanya watu kubaki kuwa watumwa katika ujira mdogo Sasa kwanini wazee wasiseme ni wavivu?
Nazani Vijana tukikubali Hali halisi kuwa sahizi zama zimebadilika ajira ni ngumu kuliko kubaki mjini kwa ujira kidogo hebu tutazame kilimo na tuwe na subira katika biashara tunazofanya na pia tupunguze kwenda na kila iitwayo fasheni maana Vijana wengi inawaharibu.

"Ni rahisi Sana maji kuyatengenezea mkondo kuliko kuyazuia"
Upvote
4