Bora wazee waliobadilishana almasi kwa shanga na vikombe sisi leo mahindi/mazao kwa makaratasi meupe!

Bora wazee waliobadilishana almasi kwa shanga na vikombe sisi leo mahindi/mazao kwa makaratasi meupe!

Uhakika Bro

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2022
Posts
3,644
Reaction score
4,315
Yas kama bei ya karatasi [hizi rimu/ream sijui] imefikia sijui 20,000s, na gharamagharama sijui thelathini naa huoni kama ni yaleyale. Ya kutoa dhahabu na kupewa kioo!!

Tunapewa kakitu kadogo tusichozalisha kwa bei kubwa na ili kupata fedha za kununulia huto tuvitu tunauza chakula chetu cha thamani kwa bei ya kawaida sana. Mahindi, alizeti..... tena kama alizeti hii ni dhahabu katika hali ya kimiminika hii mazee.

Bora hata wenzetu wa zamani walizidiwa akili na mzungu, sisi sasa tutawaambiaje wanetu? Manaake hii teknolojia waafrika pia wanaimudu, hata sisi nasikia tushawahi kuitumia -Mgololo huko. Mitoto mitundu lazima itatuulizaga tu ' Eti babaa, ni kweli mlikuwa mnauza gunia la mahindi mpate karatasi tatu za kuandikia?

Misitu ipo, kiwanda sina hakika ila mazingira yapo kwanini tusizalishe mdogomdogo. Kama teknolojia haijakua sana tuzalishe hata rimu za khaki ijulikane kwamba rimu za Tanzania wanatumiaga za ubluubluu au kaki kama hatujaweza hizo nyeupe pee! Kwa baadaye tutaziwezea tu.

Hata kama hatujaupokea na hatuutaki mojakwamoja ujamaa wa Nyerere kile kipande cha mwisho cha self reliance asee muhimu sana kama nchi. Muhimu sana nawaambia sio cha kupuuzia hata kidogo.
 
Toa pesa ya michango mzee umpelek mtoto shule, acha kulialia
 
Itasikitisha sana, endapo hizi taarifa zitakua na ukweli...
 
Back
Top Bottom