ItsMi
Member
- Sep 13, 2021
- 66
- 31
Habari zenu wadau wangu naamini sote tuwazima wa afya.
Leo tutazungumzia kwa kifupi kwa mzazi /mlezi/ndugu jamaa au rafiki kwa jinsi ambavyo unaweza kuboresha au kustawisha afya ya akili ya mtoto, kwanza kabisa afya ya akili ni vile namna ambavyo akili inamruhusu mtu kufanya matendo yanayokubsliwa na jamii pia akili kuwa na uwajibikaji madhubuti katika kupanga na kuamua mambo na kuyatimiza kwa namna yalivokusudiwa na mhusika pamoja na jamii
Tukiangalia kwa ukaribu tunaina hasa Wazazi wengi wamekuwa wakiwanyima watoto zao fursa au nafasi ya kucheza na kufurahi pamoja na wenzao auNa unaweza ukakuta mtoto anahimizwa muda wote awe kajifungia mlango ndani akiwa anaendelea kujisomea Wakati pengine huo muda ni wa wenzake kujumuika nae ili kufurahi na kama tujuavyo furaha ndiyo msingi wa afya bora.
Pili mzazi anatakiwa ahakikishe watoto wanalala mda wa kupumzika kwa watoto zao hasa pale wapowaona kuchoka inatakiwa waogeshswe wapumzike kwa lengo la kupumzisha akili ya mtoto,
Pia mtoto anatakiwa apewe mlo kamili kwa ajili ya afya yake ikiwa pamoja na kuchochea mzunguko mzuri wa damu na kumpatia vyakula kama samaki na vyakula vyenye vitamini mbalimbali pia kumpatia matunda mbalimbali kama parachichi kwa ajili ya afya ya ubongo Ikiwa pamoja na kumpatia vyakula vyenye chumvi ya madini joto. Naamini hii itapelekea utendaji bora wa afya ya mtoto
Pia tunajua kwamba wazazi waliowengi wamekuwa wakiwapiga watoto zao kwa makosa mbalimbali wanayoyafanya, Lakini pia inabidi kuchunguza hili pale mtoto anapokosea mpe nafasi ya kujitetea usimpige kabla hajajieleza kwa kuwa akizoeshwa kuadhibiwa kabla ya kujieleza usishangae akiwa kijana mkubwa tu akawa anashindwa hata kujitetea pale panapomstahili haki.
Hiyo yote inatokana kuvunjika kwa msingi bora na vile malezi aliyopitia akiwa bado mdogo. Leo nimeona niongee hili kwa kuwa watoto wa leo ndilo taifa la kesho. Hivyo mabadiliko ya kesho yanaanza na wewe,
je, Umejipangaje kwa hili.
Asante

Upvote
1