gorretti54
Member
- Jun 21, 2012
- 53
- 17
Hapana haujanikera ila umenifurahisha sana tu. Ni asilimia kubwa sana ya watanzania wanawaza kama wewe. Tatizo ni haujaelimishwa vya kutosha. Hata yule mwanakijiji wa ndani ndani kabisa ukimpa option ya kutolewa busha lake kwa operation au kubaki hivyohivyo ataamua kubaki hivyo hivyo tena atakuporomoshea matusi yanayokera zaidi. Ila wewe wa kimjinimjini ukipata busha unajua tu ni operation ndogo mtu unakuwa fit. Tofauti yenu ni uelewa. Hivi unavyotumia simu yako ya touch screen huwa hujiulizi kuna utafiti gani umefanyika nyuma yake mpaka kikatokea hicho kijisimu au huwa unatumia tu? Ukifanya uchunguzi utagundua kwamba hizi badhaa zimefanyiwa utafiti wa hali ya juu na zimekuwa approved na vyombo vinavyotambulika Kimataifa. Kimsingi vimepitia reasearch kubwa labda kupita hata hiyo touch screen phone yako unayoithamini kiwango chake. Mimi nimeweka habari njema hapa , mwenye interest anaweza akaangalia, asiyependa basi . Unaweza ukaona hivi ni sumu lakini kuna watu vimewatoa kitandani wakiwa hoi bin taaban kwa muda mfupi tu. Sasa kama wewe umeamua kumpiga mswaki mtoto wako na dawa zetu zenye fluoride ambazo zinang'arisha meno kwa kuyakwangua na ikimezwa ni hatari , au kama umekuwa unatumia antiperspirants deodorants zenye aluminium kwa maisha yako yote au kama mke wako anatatumia lipstick ya kichina yenye rangi zisizojulikana zimetoka wapi ukaona haulishwi sumu mchana kweupe tuache sisi tutumie bidhaa za aloe vera ambayo hata mababu na mababu zetu wamekuwa wanaitumia kutokana na ubora wake. Usisikilize maneno ya watu mara oh hao freemasons mara hivi mara vile. Fanya utafiti wa kina.Peleka huko hizo takataka. Samahani kama nimekukera. Watanzania tuna uzoefu wa kutosha wa hao akina GNLD, Forever Living na bra bra....WIZI MTUPU! Serikali dhaifu hadi watu wake wanalishwa sumu mchana kweupe in the name of supplements!
Ndebile, bado tunarudi kulekule kwenye ignorance. Tatizo lako ni kwamba haujaelimishwa. Tatizo lingine inaonekana umejijengea ngao fulani kwa sababu zako mwenyewe ili tu usielimike na hili. Hata mimi hapa nina mmea wa aloe vera na nilikuwa ninautumia mara mojamoja kwa kutengeneza juice kwa kutoa ile gel ya ndani na kuichanganya na matunda mengine. Lakini ndugu yangu ,unajua unatumia aloe vera ya aina gani? Kuna zaidi ya aina 200 za aloevera . Na ni moja tu inayosimama juu ya aina zote kwa kuwa na virutubisho vingi nayo ni Aloe vera barbadensis ambayo ndiyo inatumika kutengeneza bidhaa za Forever Living. Jinsi inavyopandwa na kuvunwa kwenye maelfu ya ekari yanayomilikiwa na Forever Living ni somo jengine linalohitaji muda wake.Kweli umesomea marketing, yaani hata mteja mtalajiwa akutukane....Samahani mkuu, mimi nimekulia kijijini na bado naishi kijijini, kuna mambo mengine huitaji kuwa na elimu ya juu ili kuyaelewa bali logic, instincts, and common sense.
Hivi kwenye kutafuta pesa unadhani afya ya mtu ni jambo la kipaumbele? Njia rahisi ya kuondoa sumu mwilini sio kutumia sumu,alovera iliyolimwa kwa ajiri ya biashara na ile iliyoota kwetu Bumyengeja zina ingridients sawa? Nikienda porini nikachuma majani yangu ya alovera ni sawa na hayo unayouza ambayo lazima yawe na presertative nk... Uzungu wa kudhani kutumia packed product ndio kwenda na wakati.