Borussia dortmund bingwa wa dfb pokal

Borussia dortmund bingwa wa dfb pokal

tc_edo

Senior Member
Joined
Apr 9, 2021
Posts
123
Reaction score
98
RB leipzig, timu ambayo ipo na msimu mzuri kabisa (2020/2021) na ikiwa inashika nafasi ya pili katika ligi kuu nchini Ujerumani (BUNDESLIGA) imeambulia kipigo cha goli 4-1 kwenye fainali ya DFB POKAL kutoka kwa mahasimu wao Borussia Dortmund iliyopigwa jijini Berlin, Ujerumani. Jadon Sancho (5',45+1') na Herling Braut Haland (28',87') ndo wafungaji mabao kwa BVB huku Daniel Olmo (71') akiipa RB leipzig goli la kufutia chozi.

Mtanange ulikua mkali sana maana timu hizi zimekutana May 8, 2021 kwenye BUNDESLIGA ikiwa ni wiki moja iliopita na BVB ilibuka kwa ushindi wa goli 3-2. BVB haikua na nyota wake Erling Haland kwenye hii mechi.

RBLZ ndo timu iliyo na safu bora ya ulinzi kwenye ligi kuu nchini Ujerumani msimu huu (2020/2021) ila hilo halijaitatiza BVB kuipa vichapo vinne, mara nne walizokutana.

Msimu ujao Kocha wa RBLZ; Julian Nagelsmann atatimukia Bayern Munich kuchukua nafasi ya Hans Flick kocha wa sasa wa FCB (FC BAYERN). Na pia Dayot Upamecano beki wa kati wa RBLZ nae atatimukia Fc Bayern munich kuziba pengo la Alaba aliesaini kuitumikia Real Madrid msimu ujao. Pia Boateng ambae hatakua na Fc Bayern munich msimu ujao.


Matokeo mengine Alhamis, 13 Mei 2021

EPL
Manchester United vs Liverpool 1-4
Aston villa vs Everton 0-0

La liga
Granada vs Real Madrid 1-4
Real Valladolid vs Villareal 0-2
Eibar vs Real betis 0-0

Serie A
Crotene vs Hellas verona 2-1
IMG_20210514_023830.jpg
IMG_20210514_030011.jpg
1200px-2019-07-12_Fu%C3%9Fball%3B_Freundschaftsspiel_RB_Leipzig_-_FC_Z%C3%BCrich_1DX_1124_by_S...jpg
 
Back
Top Bottom