Bosi wa zamani wa Diamond na Rich Mavoko atumbuliwa Kaburu Records

proxy

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2016
Posts
1,479
Reaction score
1,348

Kaburu (wa kwanza kulia) akiutambulisha uongozi wake mpya wa Kaburu Record

Uongozi wa ‘Kaburu Records’ studio ya kisasa iliyozinduliwa miezi mitatu iliyopita na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi, imemtimua aliyekuwa meneja wa studio hiyo Msafiri Peter ‘Papa Misifa’ kwa madai ya kushindwa kufikia malengo ya kampuni hiyo.
Soma:Jay Moe Afunguka kuhusu kutoka kimapenzi na Shilole
Akiongea Jumanne hii, Mmiliki wa studio hiyo, Kaburu, amesema wameamua kuachana na bosi huyo wa zamani wa Diamond na Rich Mavoko kutokana na kushindwa kuifikisha kampuni hiyo sehemu ambayo waliafikiana.


“Kaburu Record kama kampuni tumeamua kumsimamisha kazi Msafiri Peter ‘Papa Misifa’ kutokana na kushindwa kuifikisha kampuni yetu sehemu ambayo tulipanga,” alisema Kaburu. “Miezi mitatu sio mingi toka tumtangaze lakini kama kampuni kuna vitu ambavyo tulivipanga kuvifanya ndani ya muda huo lakini mpaka sasa hakuna dalili yoyote ya utekelezaji, hii ni biashara tumewekeza pesa ili izalishe taratibu lakini tumeona imeshindikana,”

Soma:Nay Wa Mitego Afungiwa na BASATA....... Atozwa Faini Ya Tsh. Milioni 1
Aliongeza, “Kwa hiyo mimi kama mtu kwenye hisa kubwa kwenye kampuni hii nimeamua kumfuta kazi na kuweka uongozi mpya, Papa Misifa hayupo tena kwenye kampuni hii, ukitaka kufanya kazi na sisi njoo ofisini,”

SOURCE: UBUYU BLOG
 
Hii kali, yaani hoja inahusu Kaburu lakini link zilizowekwa za watu wengine. Kweli kua uyaone, kavuta na mbegu zake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…