Bosi wasim sijakusahau

Bosi wasim sijakusahau

LA7

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2019
Posts
655
Reaction score
2,369
Boss wasim sijakusahau kabisa, yaani wewe ulikuwa ni wakunilipa elfu 20 Nile kwa mwezi mzima, halafu chakula ni kwa mama ntilie, tena pale posta kati mtaa wa idiraghand, tena nilikuwa nafanya kazi masaa 24 yaani mchana nasambaza gesi usiku nakuwa mlinzi.

Tena hata hako kakirikuu cha kusambazia gesi ulifunga milango yote na kufuli ili hata nisiweze kulala humo, tena naikumbuka ile siku umemtuma mama yako aje anijaribu ukifikiri sikujuaga mpaka Leo,

Na ukaona haitoshi mkanifanya mfanya kazi wenu wa ndani, yaani unaniagiza nikafanye usafi halafu sharti nisiongee na wadogo zako wakike, ukifikiri ntawatongoza,

Siku ambayo sitaisahau, baba yako aliniagiza kariakoo nikanoe visu, ninunue na muhindi wa mia 5 kutokana na kulala njaa siku moja nikasema ninywe hata maji ya kandoro ya 100 cha ajabu nilipofika kwa baba yako na kumpa mizigo yake aliponidai chenji nikampa na nikamwambia mia nimekunywa maji, sikutegemea, baada ya kuniambia nimekula hela ya kampuni hivo napaswa kuirudisha na wewe ukiunga mkono kabisa.

Nilipitia mengi ndani ya mwezi mmoja japo mwezi haukuisha, ila wahindi punguzeni kutudharau sisi watanzania, mbona sisi tunawapenda tu.
 
Huyo kasimu yupo humu?

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh bosi wako na baba yake ni mafia yani shingi mia ndo wanasema umekula hela ya Kampuni
 
Hizi ni story za kusadikika.
kusadikika?dada unawajua wahindi au unawasikia tu?kuna jamaa alikuwa anafanya kazi kwenye kampuni ya wahindi,wanampa milioni 5,7,10,,anafunga kwenye kiloba au rambo anapeleka bank kwa baiskeli.
alifanya kwa miaka zaidi ya 20..siku hajaja kazini,wakampa dogo mmoja 22000/=akanunue kopo la maziwa,kufika dukani yule dogo akarudishiwa 2000/= na maziwa akaleta,wale wahindi waka kaa kikao,wakamwita wakampa 20,000/=afate maziwa,dogo akaleta maziwa,,wakajua yule bingwa anawapiga 2000/,,kesho alivokuja wakamfukuza kazi..
 
Sasa ulitaka wakae na mwizi, au sijakuelewa point yako?
 
kusadikika?dada unawajua wahindi au unawasikia tu?kuna jamaa alikuwa anafanya kazi kwenye kampuni ya wahindi,wanampa milioni 5,7,10,,anafunga kwenye kiloba au rambo anapeleka bank kwa baiskeli.
alifanya kwa miaka zaidi ya 20..siku hajaja kazini,wakampa dogo mmoja 22000/=akanunue kopo la maziwa,kufika dukani yule dogo akarudishiwa 2000/= na maziwa akaleta,wale wahindi waka kaa kikao,wakamwita wakampa 20,000/=afate maziwa,dogo akaleta maziwa,,wakajua yule bingwa anawapiga 2000/,,kesho alivokuja wakamfukuza kazi..
Sasa milion 10 ni pesa ya kuweka kwenye roba?uongo kabisa huu... au haujawahi kuishika au kuiona?

Mil 10 naenda bank bila begi wala mfuko, naweka kwenye sox na mifuko ya suruali na mtu hawezi gundua kama nina hela.
 
Wee jamaa unekariri kuwa Milioni 10 lazima zote ziwe note za elfu 10?
 
Ila Wahindi wanaupumbavu mwingi mno. Wale jamaa wangekua na uchumi mkubwa kama America na kua Superpower hii dunia isingekua sehemu salama kuishi kwa dharau zao.
 
Back
Top Bottom