DOKEZO BoT chukueni hatua kwa hawa Credit Lab (Dragon Loan) bado wanatuma SMS za udhalilishaji

DOKEZO BoT chukueni hatua kwa hawa Credit Lab (Dragon Loan) bado wanatuma SMS za udhalilishaji

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Nakumbuka hivi karibuni Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ilitangaza kufungia jumla ya Application 69 zilizokuwa zinatoa mikopo kidijitali bila leseni.

Hatua hii ilikuwa ni muhimu katika kudhibiti sekta hiyo na kulinda haki za watumiaji.

Hata hivyo, licha ya kuwepo kwa sheria na hatua za kufungia baadhi ya apps, bado kuna changamoto, kwani app ya mikopo, ya Credit Lab (Dragon Loan), bado wanaendelea kukiuka sheria kwa kutuma SMS za udhalilishaji kwa wateja wao na mpaka kwa ndugu wa wateja.

Hali hii haivunji tu haki za faragha za wateja, bali pia inaleta fedheha na mateso ya kisaikolojia kwa wahusika.

Ni wazi kuwa ukiukaji huu wa sheria unaashiria dharau kwa mamlaka na sheria zilizopo, jambo ambalo linapaswa kukemewa kwa nguvu zote.
 
Back
Top Bottom