BOT wameacha Kutoa sarafu mpya Ili ziingie katika mzunguko hili linamaana gani kiuchumi?

BOT wameacha Kutoa sarafu mpya Ili ziingie katika mzunguko hili linamaana gani kiuchumi?

Wazolee

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2018
Posts
3,183
Reaction score
3,660
Wataalamu wa uchumi mkuje mutuelezee Kwa sababu gani Bank kuu wameacha Kutoa sarafu mpya Yani 50, 100 na 200 na kufanya ziadimike katika mzunguko wa biashara

Ni kwamba Kuna ishu yoyote ya kiuchumi imewalazimu kufanya hivi au Kuna kigogo tu Fulani ameshiba ugali wake na maharage akasema sitaki kuingiza sarafu mpya katika mzunguko wa biashara

Pia hizi sarafu za Tshs 50 na Tshs 100 sio imara Yani zinashika kutu na kuharibika haraka ukiringanisha na zile za Tshs 200 hivi hawakuliona hili miaka yote wakatengeneza zenye uimara kama zile za Tshs 200 au ndio 20% na mbuzi kula Kwa urefu wa kamba yake

Ukweli ni kwamba sarafu zimeadimika sokoni na ukienda Bank kuomba chengi upewe sarafu unaambiwa hakuna maana yake ni kwamba Kuna uhaba wa sarafu katika mzunguko wa biashara hapa Tanzania
Je ! Shida nini
 
Wachumi wetu watakuja kukuambia shilingi yetu inazidi kuimarika dhidi ya dola ya Kimarekani! Lakini pia uchumi wetu umezidi kukua kila mwaka kwa asilimia 5-8 kutokana na takwimu za IMF na WB!
 
Back
Top Bottom