Kuna miaka BOT walikuwa wananunua dhahabu kutoka kwa wachimbaji wadogo wadogo. Sielewi kama bado wananunua. Ukiangalia Indicative Foreign Exchange Market Rates yao dhahabu imeorodheshwa[angalia attachment chini], napata shida kidogo na kifupisho walichotumia cha Gold (T/O) hiki ni kipimo gani wana JF?. Na je kiwango cha fedha walicho weka ndiyo bei ya dhahabu? Je wapo wanunuzi wengine wa dhahabu nchini Tanzania?