Imekuw akawaida kuona Boti inayofanya safari zake kwenda Pemba kuwa na kawaida ya kujaza Watu wengi kuliko uwezo wa Boti, matokeo yake yanaweza kuwa mabaya kwa kuwa wengi wetu tuna historia ya miaka kadhaa nyuma yalipotokea majanga na kubainika kuwa kulikuwa na idadi kubwa ya Abiria kuliko uwezo wa boti.
Hii boti ya Zanzibar 1 inaebeba abiria kiasi ambacho wengi wanakosa siti kwa ajili ya kukaa, hivyo wanalazimika kukaa chini katikati ya njia ambapo Watu wengine wanatumia kupita, hili ni jambo la hatari sana.
Mamlaka za Usafiri wa Maji, Zanzibari (Pemba na Unguja) pamoja na wale wa Bara wanatakiwa kuchukua hatua mapema kwa kuwa ukimya wao hadi siku yatakapotokea madhara utakuwa hauna faida.
Kama kuna uwezekano wa kuongeza usafiri mwingine basi hatua zifanyike wakati huu kwa kuwa uhitaji ni mkubwa na sio watu wengi wana uwezo wa kulipia usafiri wa ndege.
Wananchi wengi wenye kipato cha chini na cha kati ndio wanaotumia usafiri wa Boti kwa kiwango kikubwa, Serikali ya Rais Mwinyi isikie kilio chetu, hali ni mbaya huku kwenye usafiri wa Boti.