Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Wakati wa vuguvugu la uchaguzi wa Kenya, hadi wakati wa kampeni za uchaguzi huo, Dr William Rutto alitangaza mkakati wake kabambe wa kuwakwamua Wakenya kuagana na umasikini, ulioitwa Bottom Up, akimaanisha kuwakwamua kiuchumi Wakenya makapuku (kwa Tanzania wanaitwa wanyonge) na kuwapandisha kwenye hali nzuri.
Baadhi ya Wakenya wakamuamini na kuachana na Raila Odinga, ambaye alikuwa na nafasi kubwa ya ushindi kabla ya kutafunwa na laana kutokana na kuunga mkono udikteta wa serikali ya kikatili ya Tanzania iliyoongozwa na John Magufuli.
Cha kushangaza sasa baada ya Rutto kupata urais, akasahau haraka sana mkakati wake kwenye Bottom Up mithili ya mtu aliyelogwa ili asahau kwao, akaanza kuondoa ruzuku zilizowekwa na watangulizi wake ili kudhibiti bei ya mafuta, akidai anabana matumizi, utadhani hela za Kenya ni mali ya baba yake, bei ya mafuta ikainuka na hatimaye ikainua na bei za vitu vingine na kusababisha ugumu wa maisha ambao haukuwahi kuwepo tangu Yesu alipoondoka Galilaya.
Sasa Wakenya wamekiwasha mitaani wanataka kumng'oa.
Mungu ibariki Jamhuri ya Watu wa Kenya.