INAUZWA BOXER CC 125 (ina mwezi unaenda mwezi wa Pili) BM X

The bump

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2019
Posts
1,488
Reaction score
2,908
Hii pikipiki nilininunua TAR 5 mwezi wa 9 nita attach risiti ya Manunuzi.

Pikipiki sina namna naweza ielezea, "ni mpya"

Naiuza sio kwa shida hivyo mteja apatikane asipatikane yote kheri.

Sababu ya Kuiuza ni kutokana na ngekewa ambayo imenitokea bila kutarajia, sikua nimetarajia kabisa kupata hela ya kununua usafiri nilioutaka mapema hivi.

Hatimae nimepata nikaona kuliko ning'ang'anie kubaki nayo niwe naipaki muda wote ni heri ni IUZE tu.

Hii Piki Piki imetembea KM 1670 nimemwaga OIL mara 1 tu tangu ni itoe dukani.




Chombo kimenigharimu vitu vingi kama kinavyoonekana.

Nimebadilisha vitu vingi vilivyokuja na pikipiki, TAA za mbele nimebadilisha nimefunga SPORTLIGHT kweli.

Nikikutandika FULL usiku lazima upunguze Mwendo.

Nisiisifie sana bwana pikipiki inajiuza yenyewe hiyo.

Bei yaanunuzk ipo kwenye RISITI,

Lakini kutokana imeshazoeleka BONGO kitu kikishakua mkononi ni USED basi acha nipunguze Bei naiuza hiyo pikipiki Milioni Mbili na Laki 5.

Yani 2.5M ndio bei ya hiyo Pikipiki, haina udalali ninaeandika hii post ndio muuzaji.

Kwa alie serious Karibu PM,bei haipungui na tafadhali kama hauna 2.5m usije PM, staki kumjibu mtu vibaya nasisitiza kama huna 2.5m usije PM.
 
Hii pikipiki nilininunua TAR 5 mwezi wa 9 nita attach risiti ya Manunuzi.

Pikipiki sina namna naweza ielezea, "ni mpya"
Mmh!!! mimi na juaga piki piki ni bei kweli kweli, Kumbe sio hata kwènye 5m yangu napata mbili loh! lakini kwanini hao boda boda wana tukejeli na matusi sana sisi wenye vigari vya baby walker, wakati hata robo ya bei hawafiki loh!!!!
 
Mmh!!! mimi na juaga piki piki ni bei kweli kweli, Kumbe sio hata kwènye 5m yangu napata mbili loh! lakini kwanini hao boda boda wana tukejeli na matusi sana sisi wenye vigari vya baby walker, wakati hata robo ya bei hawafiki loh!!!!
Kuna pikikipi za bei ila sio Hizi boxer zetu na tvs.

hao wanaokejeli ukute pikipiki zenyewe za mkataba
 
Uza milioni 2 wewe upate hela ya haraka! Msimu wa sikukuu na ada za shule unakaribia.
 
So ikatokea mtu akawa na pungufu utamjibu vibaya??
Wabongo biashara ndo maana huwa inatushinda

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Umeipamba sana mpka imepoteza uhalisia wake wa upya
 
Hapo Bado sana Curie, nataka next week kwenda ifanyia Sticker branding ili ibadilike kabisa, maana hapo ilipo inaonekana kama BODABODA tu. Nataka kuibandika sticker kila mahali.

Umeipamba sana mpka imepoteza uhalisia wake wa upya
 
Mkuu unaiuza kibabe sana.hiyo siyo biashara Sasa.
 
Mkuu unaiuza kibabe sana.hiyo siyo biashara Sasa.
Tanzania tumezoea sana kubembelezana,

Mkuu pamoja na ubabe huu,kuna wastarabu wengi ambao sijui ni hawakusoma Thread yote wamekuja PM kutaka pkpk kwa bei pungufu.

kutokana na ustarabu wao na namna wanavyoanza kuwasiliana na wewe mnamalizana tu kistarabu inashindikana hivyo.

Nikusihi hata wewe mkuu,ukiona biashara unabembelezwa sanaa "shtuka" Tuwe kama Wahindi.
 
Kula milioni moja nitume kijana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…